Dua ya pamoja kuwaswalia wazee


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein kulia, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma katikati, Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakisoma Dua ya pamoja kwenye eneo la Makaburi ya Wazee baada ya kumaliza kusoma Hitima maalum iliyoambatana na Maulid yanayosomwa kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Uguja jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha kulia, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salmin Amour katikati, na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, wakisoma Hitima maalum ya kuwaombea Wazee mbalimbali waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika jana katika msikiti wa kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi wa kwanza kushoto, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa pili kushoto na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, wakisoma Dua ya pamoja baada ya kumalizika Dhifa maalum ya Maulid ilioyoandaliwa na Dk. Salimin Amour, inayofanyika kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana.

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa kwanza kushoto, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour wa pili kushoto, Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi wa pili kulia, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma, wakielekea kwenye eneo la Makaburi ya Wazee walitangulia mbele ya Haki mara baada ya kusoma Hitima maalum kwa ajili ya Marehemu hao katika Msikiti Mkuu wa kijiji cha Kidombo uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana, ambapo Dua hiyo iliambatana na Maulidi ya nayayosomwa kila mwaka kijijini hapo. Amour Nassor (VPO)

Comments

Anonymous said…
komandoo naona koti limekuvaa

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri