Friday, July 11, 2008

Bunge letu bwana


HAWA jamaa wa hili Bunge letu wa ajabu sana maamuzi yao pia ya ajabu ajabu hebu cheki uamuzi wao huu wa Tume ya Huduma za Bunge na Kamati ya Uongozi juu ya uchunguzi wa kuwapo kwa madai ya kumwagwa kwa unga kwenye ukumbi wa taasisi hiyo ambao sasa unamfunga mdomo Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.

Chenge ambaye aliapa kupambana hadi hatua ya mwisho kusafisha jina lake kwa kile alichodai kuhusishwa na tuhuma za kumwagwa kwa unga huo kwenye Ukumbi wa Bunge, sasa hataweza kufanya lolote baada ya uamuzi uliotolewa jana kwamba, suala hilo limefikia ukomo na kwamba yeyote atakayezungumzia suala hilo kwa nia ya kudhalilisha Bunge au Spika atachukuliwa hatua.

Baada ya kuibuka kwa taarifa za kumwagwa kwa unga huo uliodhaniwa kwamba ni sumu ya kisasa, huku wengine wakihusisha na masuala ya kishirikina, Chenge alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kwamba, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alikuwa amemchafulia jina lake kwa kumhusisha na tukio hilo.

Chenge alisema kwamba, alikuwa na njia tatu za kupambana kudai haki yake, kwanza kulitumia Bunge; au kamati ya haki, wajibu na maadili ya Bunge au hata kwenda mahakamani kusafishwa jina lake. Soma Mwananchi kwa habari zaidi.

1 comment:

Anonymous said...

Hiyo Bunge imejaa juju!

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...