Thursday, July 10, 2008

Askofu Mokiwa mkali mno kwa mashoga


ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Nchini, Valentino Mokiwa, amesema anatamani kukalia kiti cha Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo duniani, Rowan William angalau kwa siku tatu ili aweze kutokomeza ushoga ndani ya kanisa hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mokiwa alieleza nia yake ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo ulimwenguni, utakaofanyika katikati ya mwezi huu nchini Uingereza, huku nchi za Nigeria, Rwanda, Uganda na Kenya zikiwa zimetangaza kutoshiriki.

“Wengi walitazamia kiongozi wetu atoe kauli ya kuwatimua mashoga, alitakiwa kushika hatamu na kuonyesha njia…, kama ningepewa kiti chake angalau kwa siku tatu tu, ningewatimua mashoga na ninaamini tabia hii ingekoma, kwa sababu inakwenda kinyume na maandiko ya Matakatifu ya Mungu tunayemwamini,” alisema Mokiwa.

Alisema yeye ni miongoni mwa maaskofu wakuu 38 wa kanisa hilo duniani na kwamba, ingawa ndiye mdogo kuliko wote kiumri, alishamuandikia barua Askofu Mkuu wa Canterbury kumuomba awashughulikie wanaojihusisha na vitendo vya ushoga. Imeandikwa na Editha Majura.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...