Thursday, June 30, 2016

MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan(kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia)mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengenezakipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba  wakati wa tafrijaya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima  iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.

KONGAMANO LA KUBADILISHANA UZOEFU WA MAFUNZO YA TAALUMA UFARANSA NA TANZANIA LAFANYIKA


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak.
(Picha na Modewjiblog)
 
Taasisi ya utoaji mafunzo ya Ufaransa ya AFPA ndiyo ilikuwa inaendesha mafunzo hayo wakibadilishana uzoefu na wadau wa Tanzania kutoka sekta binafsi.
Akifafanua zaidi Dkt. Kida alisema kwamba kongamano hilo limelenga zaidi katika kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto zinazojitokeza na fursa zilizopo katika mafunzo, ukuzaji na uendelezaji taaluma.
Dkt. Kida alifurahishwa na mchanganyiko wa watu kutoka sekta binafsi waliofika katika kongamano hilo ambao aliamini kwamba wataelezea uzoefu wao katika kukabiliana na changamoto za taaluma katika makampuni yao.
Aidha alisema kwamba wadau hao wa Tanzania watapata uzoefu wa timu ya wataalamu wanne kutoka kwa wakala wa mafunzo ya taaluma nchini Ufaransa (AFPA) ambao wataeleza miaka 60 ya uzoefu katika masuala ya mafunzo ya taaluma na uendelezaji wa utaalamu.
 Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kushoto) akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
 
Alisema anaamini kwamba mchanganyiko huo wa wadau utasaidia katika kukabiliana na tatizo la taaluma katika soko la ajira la Tanzania.
Alisema mazungumzo hayo ni muhimu sana katika kuibua fursa hasa wakati taifa hili linajipanga kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda na bila wataalamu wenye taaluma zao makamapuni na viwanda vingi vitakuwa na shida kubwa.
Alisema changamoto kubwa inayokabili taifa la Tanzania kuelekea nchi ya viwanda kama ilivyo katika nchi nyingine zinazoendelea ni ukosefu wa taaluma na utaalamu.
“Ukosefu wa wafanyakazi wenye taaluma katika ngazi zote ni tatizo kubwa linalokabili harakati za kuelekea uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Kida.
Anasema pamoja na matatizo hayo taasisi yake tayari imeshaanza kushughulikia shida hiyo ya taaluma nchini Tanzania kwa kuwa na makongamano mbalimbali makubwa yanayokutanisha wadau kuzungumzia hali hiyo.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kushoto) alipowasili ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.
 
Alisema kwa mfano mwaka 2015 iliendesha jukwaa la mafunzo ya ufundi (VTEC) Africa. Katika jukwaa hilo lililofanyika Machi 10 -12 mwaka huo walizungumzia mafunzo ya utaalamu wa gesi na mafuta kwa mataifa ya Afrika. Jukwaa hilo liliendeshwa kwa kushirikiana na kampuni ya Uingereza ya Getenergy.
Aidha Oktoba 9, 2015 iliendesha semina kuhusu uumbaji wa programu za mafunzo kwa aili ya kupata wataalamu wa gesi na mafuta.
Lakini, alisema, kuanzia Julai 2014, ESRF imekuwa ikishirikiana na shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kutekeleza mpango wa miaka mitano wa mafunzo ya kinadharia na utaalamu yenye mfumo wa Ushiriki ambapo ESRF yenyewe hutoa msaada wa kitawala na lojistiki kwa wanafunzi ili waweze kwenda kuhudhuria mafunzo nje ya nchi.
Aidha ESRF imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali na uchambuzi kuhusiana na uendelezaji wa taaluma nchini Tanzania na moja ya ya tafiti hiyo ni kudorora kwa ubora wa elimu Tanzania na namna ya kuzuia anguko hilo na kulibadili.
Mwaka 2014 na mwaka huu kuna mada inayozungumzia uendelezaji wa mafunzo ya taaluma na uwezo wa uzalishaji Tanzania.Mada hii ni sehemu ya taarifa ambazo zitapatikaa katika ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kulia) akiongozana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF. Nyuma ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi pamoja na Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki.
KONGAMANO kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa makampuni na viwanda.
Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Wengine waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.

LAPF NDANI YA MAONESHO YA SABASABA 2016

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za ushiriki wa Mfuko katika maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
L2Afisa Mifumo ya kompyuta kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili akitoa maelezo kwa mwanachama wa Mfuko pamoja na kumpatia taarifa ya michango yake mara baada ya mwanachama huyo kutembelea banda ya Mfuko kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).

GAZET LA MTANZANIA LA ZINDUA MWEONEKA MPYA “MTANZANIA LIMEBORESHWA

005Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa  Mtanzania, Dennis Msacky na Meneja Masoko wa kampuni hiyo.
????????????????????????????????????Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Dennis Msacky.akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”Katikati ni Mhariri Mtendaji Kampuni ya New Habari(2006)Ltd, Absalom Kibanda na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Michael Bugidira.
Picha na Mpiga Picha Wetu

WAFANYAKAZI NHC WAFANYA HAFLA FUPI KUMUAGA MSTAAFU MAMA CLARA NGALIOMA

Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Agatha Makungu akimkabidhi zawadi ya seti ya vyombo mbalimbali vya kupikia Mama Clara Ngalioma aliyetumikia Shirika la Nyumba kwa uadilifu mkubwa kwa kipindi cha takribani miongo mitatu na kustaafu rasmi jana. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
Mama Clara Ngalioma aliyetumikia Shirika la Nyumba kwa uadilifu mkubwa kwa kipindi cha takribani miongo mitatu na kustaafu rasmi jana akilengwa lengwa na machozi ya furaha baada ya kukutana na wafanyakazi wenzake waliomuaga kwa upendo. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
 Picha ya pamoja ya Mama Clara Ngalioma na wafanyakazi wenzake. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
 Picha ya pamoja ya Mama Clara Ngalioma na wafanyakazi wenzake. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.

Picha ya pamoja ya Mama Clara Ngalioma na wafanyakazi wenzake. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.

 Wafanyakazi wenzake wakimpelekea zawadi hiyo jana jioni. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
 Mama Clara akitakiwa kila la kheri na mmoja wa wafanyakazi wenzake Swahiba Msuya jana jioni huku wengine wakishuhudia.
 Picha ya pamoja ya Mama Clara Ngalioma na wafanyakazi wenzake. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
 Picha ya pamoja ya Mama Clara Ngalioma na wafanyakazi wenzake. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.
Picha ya pamoja ya Mama Clara Ngalioma na wafanyakazi wenzake. Hafla fupi ya kumuaga Mama Clara ilifanyika jana jioni Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF KUTOA HUDUMA ZOTE KWA WATEJA WAKE VIWANJA VYA SABASABA

Muonekano wa nje ya Jengo la PPF lililopo Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar esSalaam (Sabasaba).
 Maandalizi
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally (katikati) na Afisa Michango Glory Maboya, wakijiandaa kuhudumia wateja leo asubuhi katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
 Afisa Utafiti Neema Mjema (nyuma) na Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka, pia wakijiandaa kuweka mambo sawa kabla ya kuanza kupokea wateja katika Bandao lao la Maonesho kwenye Viwanja vya Sabasaba leo.
 Afisa Uwekezaji wa Mfuko huo, Jonas Mbwambo akiweka mambo sawa kabla ya kuanza kupokea wateja katika Banda lao namba 86 viwanja vya Saba saba.
 Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Pauline Msanga, akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Huduma za uendeshaji Mfuko huo, wakati walipotembelea katika Banda lao lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, leo. 
 Sehemu ya wananchi waliotembelea Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF wakipata elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko huo na jinsi mwanachama anavyoweza kujiunga na kuchangia.


WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...