Taarifa zilizopatikana hivi punde ni kwamba Basi la abiria la kampuni ya Luwinzo , lifanyalo safari zake Dar-Njombe inaelezwa kuwa limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar kwa kuligonga Lori , kwa taarifa za awali ambazo bado hazithibitishwa na jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kuna vifo vya watu kadhaa, ambayo idadi yake haijajulikana mpaka sasa sambamba na majeruhi.
TUTAZIDI KUPEANA TAARIFA ZAIDI KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZIKIPATIKANA.
Baadhi ya Abiri na Wasamalia wema wakisaidia kuwaokoa baadhi ya abria waliokuwa wamenasa ndani ya basi hilo.
Baadhi ya abiria wakiwa kwenye masikitiko makubwa.
Kazi ya kuokoa baadhi ya abiria ikiendelea
Namna basi hilo lilivyogonga Lori kwa nyuma.
No comments:
Post a Comment