Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uongozi kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi Mussa Mandia katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi zawadi ya kuhitimu mafunzo ya uongozi kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi Prisca Lyimo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Faustine Masalu akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafuzo ya kutoka mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.
Shirika la Hifadhi za Taifa limeanza rasmi kutumia mfumo wa jeshi usu kutoka ule wa kiraia katika utendaji kazi wake ikiwa ni hatua mojawapo ya kuongeza ufanisi katika shughuli za uhifadhi.
Jumla ya wahifadhi 40 walihitimu mafunzo ya Awamu ya kwanza ya kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu kwa kwa viongozi maafisa wa ngazi ya kati “Transformation Leadership Course for Middle Cadre Wardens” yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi hivi karibuni.
Mfumo wa utendaji kazi kwa kijeshi-usu utalisadia shirika kuimarisha nidhamu ili kuboresha utendaji kazi hasa katika nyakati hizi ambapo changamoto kuu ya ujangili unaotumia silaha za aina mbalimbali za moto hasa za kivita inazidi kushika kasi.
No comments:
Post a Comment