Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Meneja Mkuu wa Tigo kuzungumza na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa chapa mpya yenye kauli mbinu ya ‘Live it, love it’ itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigitali nchini. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez, akionesha simu mpya zenye menyu ya Kiswahili wakati wa mkutano huo.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Olivier Prentout (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu huduma mpya za Tigo kuelekea Sikukuu ya Krismas.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
……………………………………………………………………….
Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo, imezindua chapa mpya yenye kauli mbinu ya ‘Live it, love it’ itakayoimarisha nafasi ya mbunifu anayeongoza kwa ubunifu wa kidigitali nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapa hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez alisema chapa hiyo mpya itahakikisha inakuwa rafiki nzuri kwa Watanzania kuziona ndoto zao na kuzifikia.
Alisema kwa hapa nchini kama zilivyo nchi zingine intaneti imekuwa nisehemu muhimu ya maisha ya watu kutokana na huduma za kidigitali kutumika katika biashara, elimu, kwa familia na kwa kujiburudisha.
“Tumejikita kwenye utoaji huduma katika matarajio hayo na rekodi ya mwenendo wa ubunifu wetu unatupa imani kuwa tunafanikiwa,” alisema Gutierrez.
Katika hatua nyingine, kampuni hiyo imetoa ofa kwa wateja wake kwa kuuza simu ya smartphone ya aina ya Tecno Y3 kwa sh. 99,000 kuelekea msimu wa Sikukuu ya Kristmass na Mwaka Mpya.
Gutierrez alisema simu hiyo itakuwa na ‘menu’ ya Kiswahili itakayomuwezesha mteja kuitumia kwa urahisi huku ikiwa na kamera mbele na nyuma, betri linalokaa kwa muda mrefu na vitu vingine.
No comments:
Post a Comment