Tuesday, November 17, 2015

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI NA KUWAPONGEZA KWA KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU KWA AMANI NA UTULIVU

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakati wa mkutano wa Kujitambulisha na kufahamiana na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza jeshi hilo kwa kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
 Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akiwaongoza watendaji wakuu na maafisa wa jeshi hilo kuimba wimbo wa maadili wa jeshi hilo wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wapili kushoto). Ziara hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo, ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji hao. Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watendaji wakuu na Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji hao. Kushoto meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki, wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
 Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akitoa taarifa ya Jeshi hilo wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji wa jeshi hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia), akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova baada ya kumaliza ziara yake katika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve, wapili kushoto ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Musa Ali Musa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Diwani Athumani.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo ( watano kulia), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (watano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu na Maafisa wa jeshi hilo muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...