Friday, November 20, 2015

SHEREHE ZA KUAPISHWA WAZIRI MKUU WA AWAMU YA TANO VIWANJA VYA IKULU NDOGO CHAMWINO MJINI DODOMA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimkabidhi nyaraka za Serikali baada ya kumwapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpongeza Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015.
Rais Dkt. John Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, baada ya kuapishwa Waziri huyo Mkuu kwenye Viwanja vya Ikulu Ndogo Chamwino mjini Dodoma leo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...