Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Tanzania, Dk Juma Gulaid akisoma taarifa kabla ya kukabidhi vifaa vya kuhudumia watoto katika hafla fupi iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando.Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Baadhi ya wauguzi wakisimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Tanzania, Dk Juma Gulaid katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akizungumza katika hafla ya kupokea vifaa vya kisasa vya kuhudumia watoto katika hospitali hiyo. Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk Juma Gulaid.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk Juma Gulaid akimkabidhi hati ya vifaa vya kuwahudumia watoto kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akipokea hati ya vifaa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando. Vifaa hivyo vimetolewa na UNICEF.
Baadhi ya wauguzi wakisimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Tanzania, Dk Juma Gulaid katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa
………………………………………………………………………………….
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepatiwa msaada wa vifaa kumi vya tiba vya kuwahudumia watoto mara wapougua na kufikishwa kwenye hospitali hiyo.
Vifaa hivyo vina thamani ya Dola za Kimarekani Laki moja sawa na zaidi Sh milioni 2 vimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF),kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni Ventilator, medical, adult –child ,w/access pamoja na Warmer system , newborn, radiant, w/access.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk Jama Gulaid amesema mchango wa UNICEF na michango ya wadau wengine itawezesha watumishi wa hospitali ya Muhimbili kuokoa maisha ya watoto ambao wanahitaji huduma za afya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando amesema hadi kufikia mwaka 2013 Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto hao kwa theluthi mbili.
Kwa mujibu wa Dk Mmbando, mwaka 2013 Tanzania imepunguza vifo hivyo na kufikia 54 kwa vizazi hai 1,000 na kufikia lengo la Milenia na kwamba mafanikio hayo yametokana na kiwango kikubwa cha chanjo , matumizi sahihi ya dawa za Malaria pamoja na vyandarua.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru UNICEF kwa msaada huo ambao utachangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watoto na kuboresha huduma za afya .
No comments:
Post a Comment