Thursday, November 26, 2015

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAZINDUA RASMI MAUZO YA NYUMBA ZA KAWE SEVEN ELEVEN (711)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuzindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) Kawe. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Januari mwaka 2015 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo mwezi Disemba 2018, ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Wanaoshuhudia na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi (kushoto) na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa NHC, Hamad Abdallah 
                                      
Nyumba za mradi mpya wa Seven Eleven (711) Kawe zinavyoonekana zitakavyokamilika. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Januari mwaka 2015 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo mwezi Disemba 2018, ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fukwe za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuzindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) Kawe.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuzindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) Kawe. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Januari mwaka 2015 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo mwezi Disemba 2018, ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Wanaoshuhudia na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi (kushoto) na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa NHC, Hamad Abdallah 
  
 Nyumba za mradi mpya wa Seven Eleven (711) Kawe zinavyoonekana zitakavyokamilika. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Januari mwaka 2015 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo mwezi Disemba 2018, ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fukwe za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni.

Nyumba za mradi mpya wa Seven Eleven (711) Kawe zinavyoonekana kwa sasa. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Januari mwaka 2015 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo mwezi Disemba 2018, ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fukwe za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni.

Mhandisi wa Mradi wa Kawe 711, Kishor Hirani akimpa maelezo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati wa uzinduzi rasmi wa mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) Kawe kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UUZWAJI WA NYUMBA ZA SEVEN ELEVEN (711) KAWE

Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Alhamisi, 26, Novemba, 2015) limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) Kawe. Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwezi Januari mwaka 2015 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo mwezi Disemba 2018, ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huu una ukubwa wa mita za mraba 111,842.90 na unatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya Sh 187,927,105,500 mpaka utakapomalizika. Pia ikumbukwe kuwa mradi huu ni sehemu ya mji mpya wa kisasa (Satellite City) unajengwa hapa.

Mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fukwe za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay,Morocco na Mikocheni huu una jumla ya nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane tofauti ya ghorofa 18 kila moja, ukiwa na huduma zote muhimu za kijamii. Kutakuwepo pia na sehemu ya maduka kubwa kwa ajili ya wakazi na maeneo ya jirani.

Mradi wa Seven Eleven Kawe una Nyumba za aina 4 kama ifuatavyo:

S/No
Aina ya nyumba
Idadi ya nyumba
1
Vyumba viwili kawaida
 24
2
Vyumba vitatu kawaida
254
3
Vyumba vuitatu dungu
128
4
Vyumba vinne ya kifahari
 16

Jumla
422

Kwenye kila nyumba katika mradi huo vyumba vyote vimejitosheleza kwa kuwa nba maliwato (en suit), kuna sebule iliyoungana na eneo la kulia chakula, maliwato ya wageni na jiko kubwa la kisasa. Nyumba hizo zina ukubwa wa aina tofauti kutokana na idadi ya vyumba vyake, yaani zile za ukubwa wa mita za mraba 128, mita za mraba 132, mita za mraba 151, mita za mraba 182 na nyingine za ukubwa wa mita za mraba 244.

Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo kubwa la ziada la maegesho ya magari, eneo la kucheza watoto, eneo la viwanja mbalimbali (Mpira wa kikapu, mpira wa tennis), maeneo ya mbio za riadha (jogging) & baiskeli pamoja,  Club House eneo maalum la kukusanyia taka .

Bei za Nyumba katika mradi huo zitaanzia TZS 346,376,625 bila VAT. Hata hivyo, Shirika la Nyumba linapenda kutangaza punguzo la 5% kwa wateja wa mwanzoni (Early Bird) ambao watakaolipa katika muda maalumu. Nyumba zitakazowekwa sokoni kwa sasa ni Nyumba 106 tuu. Tunawahamasisha na kuwakaribisha Watanzania wote walio nchini na wanaoishi nje ya nchi wafanye mawasiliano na ofisi zetu za Makao Makuu ya Shirika, ofisi zetu za mikoa, au kupitia barua pepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato.

Uzinduzi wa mauzo ya nyumba za mradi huu ni mfululizo wa uzinduzi wa miradi ya NHC unaolenga kutimiza malengo ya mkakati wa Shirika wa miaka kumi 2015/16 – 2024/25.

Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayehitaji kununua nyumba katika mradi huu, tafadhali waweza tumia akaunti nambari 005-201-0010334-01(TZS) au 005-201-0010334-02(USD) iliyopo Tanzania Investment Bank (TIB) Mlimani City. Pia unaweza kuwasiliana na kitengo cha mauzo kupitia simu namba + 255 754 444 333, +255 784 105 200 na  +255 222 162 800; barua pepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya shirika www.nhctz.com  kwa maelezo zaidi.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...