Wednesday, November 18, 2015

BENKI YA DTB TANZANIA YAUZA HISA ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 30

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB), Viju Cherian (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu benki hiyo kuuza hisa zenye thamani ya sh. bilioni 30 na kusherehekea miaka 70 ya uwepo wake tangu ianzishwe hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa benki hiyo, Joseph Mabusi.
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa benki hiyo, Joseph Mabusi (kulia), akizungumzia mafanikio mbalimbali  na shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
 Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uzalishaji na Masoko wa benki hiyo, Sylvester Bahati (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua  taarifa hiyo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
 ……………………………………………………………………………………………………………………….
 
Benki ya Diamond Trust (DTB Tanzania) hivi karibuni
imefanikiwa kuuza hisa stahili (Rights Issue) zenye thamani ya shilingi 30
billion kwa wanahisa wake kwa bei ya shilingi 5,200 kwa kila hisa. Hii ni mara
ya tatu kwa DTB Tanzania kuuza hisa stahili ambapo mwaka 2007 iliuza hisa kama
hizo zenye thamani ya shilingi bilioni 5.3 na mwaka 2012, shilingi bilioni 12.4
 
Uuzaji wa hisa unaimarisha mtaji wa benki na kuendelea
kuwekeza kwenye matawi mapya, teknolojia na uanzishwaji wa huduma mpya.  DTB Tanzania imeendelea kukua ikianza na
matawi manne (4) mnamo mwaka 2007 wakati wa hisa stahili za kwanza hadi matawi
24 hivi sasa.
 
Mwaka huu, DTB Tanzania imezindua akaunti maalum za akiba
kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye kipato tofauti kutimiza malengo yao. Akaunti
hizi ni pamoja na Akaunti ya watoto (Smart Saver), akaunti ya akina mama
(Amani), akaunti ya wazee (Faraja) na akaunti ya wanafunzi wa sekondari na vyuo
(Kisomi Zaidi).
 
Pia uongezaji wa mtaji wa benki unakusudia kuendana na matakwa
ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), juu ya kanuni za mitaji ya mabenki. DTB
Tanzania ni benki ambayo siku zote imukuwa mstari wa mbele kutimiza matakwa ya sheria
juu ya mitaji ya mabenki ikiwa ni pamoja na ongezeko la viwango vya mitaji
(core /total capital ratios). Benki ya DTB Tanzania imekuza mtaji utakaoendena
na mipango ya kibiashara kwa miaka ijayo.
 
DTB Tanzania ambayo inasherehekea miaka 70 ya uwepo wake
Tanzania, imepata mafanikio ya kuridhisha kwa kipindi cha miezi tisa iliyoishia
tarehe 30 Septemba 2015. Faida bila kodi imefikia shilingi 20.0 bilioni; ikiwa
ni ukuaji wa asilimia 30.1 ikilinganishwa na shilingi 15.4 bilioni iliyopatikana
katika kipindi kama hicho mwaka jana. DTB Tanzania ni miongoni mwa benki chache
nchini Tanzania, zilizofanikiwa na ongezeko kabla ya faida ya zaidi ya asilimia
31 kwa miaka mitano sasa.
 
Amana za wateja imekua kwa asilimia 30 kutoka shilingi 504
bilioni Septemba 2014, hadi shilingi 720 bilioni mwishoni mwa Septemba 2015.
Mali za Benki (Total Assets) zimefikia shilingi 858 bilioni ikilinganishwa na
shilingi 632 bilioni mwezi Septemba 2014, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 26. Mali
za Benki (Total Assets) ziliongezeka kwa asilimia 24 mwaka 2012, asilimia 26
mwaka 2013 na asilimia 36 mwaka 2014.
 
 
Amana zisizo na riba (Casa deposits) zilikuwa shilingi 372
bilioni, ongezeko la asilima 40.5 toka shilingi 265 bilioni mwezi Septemba
2014. Mikopo kwa wateja ilikuwa shilingi 512 bilioni ikilinganishwa na shilingi
391 bilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2014, ikiwa ni ongezeko la asilimia
23.
 
 
Kwa sasa DTB Tanzania ina mtandao wa matawi 24 nchi nzima. Matawi
10 yakiwa Dar es Salaam (Tawi Kuu la Dar, Kariakoo, Magomeni, Masaki, Mbagala,
Mbezi, Morocco, Nelson Mandela na Upanga iliyopo barabara ya Umoja wa Mataifa. DTB
Tanzania pia ina matawi 14 kwenye miji mikubwa nchini, ikiwa ni matawi 2 jijini
Arusha, matawi 2 Jijini  Mwanza na tawi
moja moja katika miji ya Dodoma, Iringa, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi,
Mtwara, Tabora, Tanga na Zanzibar.
 
 
DTBT ni kampuni tanzu ya Diamond Trust Bank Group yenye
matawi  zaidi ya 115 katika nchi za Tanzania,
Kenya, Uganda na Burundi. DTB ni mshirika wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Aga
Khan (Aga Khan Fund for Economic Development -AKFED), ambayo ni sehemu ya Mtandao
wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network). 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...