Monday, November 30, 2015

NHIF YAKABIDHIWA KITUO CHAKE DODOMA

mi01Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha ufunguo wa kituo hicho baada ya kukabidhiwa na baadae alikikabidhi rasmi katika uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
mi1Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando akikagua Kituo cha Kisasa cha Matibabu kilichopo katika Hospitali ya Mkoa Dodoma. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka huu.
mi2Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
Makadhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla fupi
iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto
Associates.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.
Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.
Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.
Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa fedha, Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...