Saturday, September 12, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI AITEKA MUSOMA, MWIGULU NCHEMBA AWAPONDA WAPINZANI

????????????????????????????????????

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Tarime katika mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika mjini Tarime jana ambapo Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili aweze kuingia ikulu na kuwatumikia watanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko bora kwa watanzania na siyo bora mabadiliko
Naye Mwigulu Nchemba  ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi ameendelea kuwaelimisha Watanzania namna UKAWA wanavyopotosha Umma kuhusu Kauli za Baba wa Taifa. Nanukuu”Ni kweli Baba wa Taifa Mwl.Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata Mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta NJE ya CCM.”
Kauli hiyo ya Kutafuta Mabadiliko nje ya CCM ambayo ilisemwa na Baba wa Taifa ilijikita kwenye Mambo makuu 4 ambayo Watanzania wasipoyaona ndani ya CCM watakwenda kuyatafuta nje ya CCM.
Jambo la kwanza ni RUSHWA,Mwl.Nyerere alisema,Watanzania wanahitaji kiongozi anayeweza kukemea Rushwa bila kuona aibu,Rais aweze kuwambia Jamaa zake kuwa Rushwa ni hatari kwa Ustawi wa Taifa letu.Hivyo Watanzania wasipopata mtu anayepinga Rushwa ndani ya CCM watakwenda kumtafuta nje ya CCM.Swali kwa uchaguzi huu wa mwaka 2015,Mtu anayepinga RUSHWA yupo ndani ya CCM au Nje ya CCM?? Jibu ni yupo ndani ya CCM na yule mwenye sifa ya kula Rushwa na kuiba mali za Umma yupo NJE ya CCM.Hivyo Watanzania wanatakiwa kuiingua Mkono CCM na sio hao wengine.
Jambo la pili MUUNGANO, Mwl.Nyerere alisema Kiongozi Mkubwa kama Rais ni lazima autetee Muungano wa Nchi yetu.Hivyo Watanzania wasipopata Mgombea ndani ya CCM anayeweza kuutetea Muungano wetu,Watakwenda NJE ya CCM kumtafuta mtu anayeweza kutetea Muungano wetu. Swali,Kati ya CCM na Wagombea wengine ni Mgombea yupi anasera za kuutetea Muungano wetu??Rejea kauli ya Mwl.Nyerere kuwa serikali tatu(3) ni kuua Muungano wetu.
Jambo la tatu ni UDINI na UKABILA,Mwl.Nyerere alisema ,Kiongozi wa Taifa kubwa kama Tanzania ni lazima adumishe Ummoja kwa kuzuia Udini na Ukabila.Hivyo Watanzania wasipopata Mgombea Urais anayeweza kukemea Udini na Ukabila bila kuuonea haya watakwenda nje ya CCM kutafuta mtu anayekemea Udini na Ukabila.Swali,Kwa wagombea wa sasa kwenye Uchaguzi huu 2015 ni Mgombea yupi anaeneza UDINI na Ukabila na Yupi anakemea Udini na Ukabila??
Uchaguzi Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Rais , Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka hii nchini kote ukishirikisha vyamba mbalimbali vya kisiasa.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MUSOMA)
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi mjini Musoma  katika mkutano uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mkendo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake mjini Tarime.
????????????????????????????????????
Mwigulu Nchemba akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma
????????????????????????????????????
Jaji Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba akizungumza na wananchi wa mjini Tarime wakati alipokuwa akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli. 
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Tarime mkoani Mara.
????????????????????????????????????
Vijana hawa wakiwa  wamejipaka rangi CCM za mwilini mwao kama ishara ya kukipenda chama hicho.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mkendo mjini Musoma
????????????????????????????????????
Baadhi ya wazee wakipmokea Dr. John Pombe Magufuli alipowasili mjini Tarime mkoani Mara.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akipiga Drums Ngoma za muziki wakati alipofika Utegi wilaya ya Rolya na kufanya mkutano wa kampeni.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Utegi wilayani Rolya.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Rolya Mh.Okambo Lameck Airo mjini Utegi.
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa jimbo la Rolya Mh.Okambo Lameck Airo akiomba kura kwa wananchi wa Utegi huku Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimsikiliza katikati ni Mzee Jaji Joseph Warioba.
????????????????????????????????????
Makongoro Nyerere akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Musoma.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiongozana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo wakati alipowasili katika shule ya msingi Nyasurura. 
????????????????????????????????????
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika kijiji cha Nyasurura.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Jaji Joseph Warioba katika kijiji cha Nyasurura kushoto ni Makongoro Nyerere.
????????????????????????????????????
Kundi la TOT likifanya vitu vyake katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mzee Steven Wasira kulia akizungumza na Mwigulu Nchemba.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwigulu Nchema wakati alipokuwa akizungumza naye.
????????????????????????????????????
Kada wa CCM Amon Mpanju akizungumza na wananchi wa Musoma mjini wakati alipokuwa akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mzee Steven Wasira akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma.
????????????????????????????????????
Mzee Jaji Joseph Warioba  akiwahutubia wananchi wa Musoma katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.
????????????????????????????????????
Mwigulu Nchema Kulia na Makongoro Nyerere akiwateta jambo wakati wa mkutano huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Ndugu Vedastus Mathayo mgombea ubunge jimbo la Musoma mjini CCM akiwaomba kura wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukinyoosha mikono yao juu kuashiria kumkubali Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Uwanja wa Mukendo ukiwa umejaa wananchi.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiondoka huku akiwapungia wananchi mkono mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika uwanja wa Mukendo mjini Musoma.
????????????????????????????????????
Wananchi nao wakimpungia mikono kuashiria kumuaga.

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...