Wednesday, March 31, 2010

Rais apokea ripoti ya CAG




RAIS Jakaya Kikwete amepokea ripoti za Ukaguzi wa Matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake za mwaka 2008/2009 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Utouh.

Ripoti alizopokea Rais ni za Ukaguzi wa Taarifa za Fedha ambazo zinahusu Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na za Mashirika ya Umma.

Ripoti zingine ni za Ufanisi ambazo ni ripoti ya jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi, ukaguzi wa ufanisi na thamani ya Fedha kwenye sekta ya ujenzi wa Barabara.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyorekebishwa mwaka 2005, pamoja na sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 iliyorekebishwa mwaka 2000, mara baada ya kupokea ripoti hiyo anatakiwa kumwagiza Waziri mwenye mamlaka husika kuziwasilisha ripoti hizo Bungeni.

Katika mazungumzo hayo Utouh amemueleza Rais Kikwete juu ya mafanikio mbalimbali ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka mwaka 2005/2006 hadi za 2008/2009 na kuonyesha kuridhishwa nazo.

Baadhi ya mafanikio hayo ni uwezo wa ofisi yake kuwakilisha ripoti nne kwa mwaka huu 2008/2009 kutoka ripoti mbili mwaka uliopita wa 2005/2006.

Itakumbukwa kuwa Ripoti za mwaka 2005/2006 zilijadiiwa chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete katika vikao muhimu vitatu ambacho ni kikao cha Baraza la Mawaziri, Kikao cha viongozi wakuu wa Serikali Kuu kilichofanyika na kikao cha Viongozi Wakuu wa Serikali za Mitaa vyote vilifanyika Aprili , 2007.

Bwana Utouh pia ameeleza kuwa tofauti na ripoti za mwaka 2005/2006 ambazo uandaaji wa taarifa za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa ulitumia viwango na miongozo ya ndani ya nchi, uandaaji wa ripoti hizi mpya umetumia viwango vya kihasibu vya Kimataifa.

Hatua nyingine kubwa iliyofikiwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni kuwa ukaguzi wa Balozi za Tanzania za ripoti iliyopita ulifanyika kwa kutumia sampuli chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati ripoti hii ya leo ukaguzi umefanyika kwa Balozi zote na kila Balozi kupewa hati yake ya Ukaguzi na katika ukaguzi mzima hati za mwaka huu zinaonyesha kuboreka zaidi kuliko za kipindi kilichopita.

Akipokea Ripoti hizo Rais Kikwete aliishukuru ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi hiyo na kuahidi kuijengea ofisi hiyo ili ifanye kazi vizuri zaidi.

“ Tutafanya jitihada ya kuwawezesha zaidi, ni muhimu kuongeza watumishi, mishahara, vitendea kazi ili mfanye kazi vizuri zaidi”.

Alisema Rais na kusisitiza kuwa nidhamu kwenye matumizi ya fedha ni muhimu na kwamba tangu serikali ilipoelezea na kukuza uelewa na umuhimu wa nidhamu katika matumizi ya fedha kwa viongozi na watendaji, nidhamu imeanza kuonekana na hivyo hakuna budi kujenga nidhamu zaidi.

Tigo sasa yaja na Sumni kupiga simu


Kulia ni Meneja Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando na kushoto ni Meneja matangazo na promosheni Redemtus Masaja akizindua Rasmi viwango nafuu vipya vya mawasiliano kwa wateja wa Tigo kuanzia kesho. Ukiwa Tigo Thumni inathamani kama zamani!Ongea utakavyo, sasa ni nusu shilingi kila sekunde baada ya dakika ya kwanza,saa20 kwa siku, kasoro saa12jioni-4usiku.Tigo

Mrisho Mpoto ndani ya Bakita



Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mrisho Mpoto, akitumbuiza katika uzinduzi wa Baraza la Kiswahili Taifa(BAKITA),uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga.

Tuesday, March 30, 2010

YALIYOJIRI UZINDUZI KITABU CHA SIR GEORGE





Mambo kibao yalijiri wakati Rais Jakaya Kikwete alipozindua kitabu kiitwacho ‘Sir George’ Ijumaa iliyopita kilichoandikwa na mtoto wa Balozi, George Kahama katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Marais wastaafu wa awamu ya pili na ya tatu yaani Alli Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa walikuwapo kwa upana zaidi na wakashiriki katika tukio hilo kwa kina mbali na viongozi hao piwa walikuwapo viongozi maarufu waliopata kuwapo katika awamu zote tangu ya kwanza.
Kitabu hiko kinachoeleza historia ya Tanzania kupitia miaka 50 ya utumishi wa Kahama, kilianza kuandikwa mwaka 2006 na utangulizi wa kitabu hiko umeandikwa na Rais Kikwete.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Kikwete alitoa wito kwa watu wa matabaka mbalimbali kujenga tabia ya kusoma vitabu na kuandika vitabu vinavyohusu masuala mbali mbali nchini.
“Ninafarijika kuzindua kitabu hiki cha Sir George kutokana na ukweli kwamba kitabu hiki kitakuwa cha manufaa kwa taifa letu, kutokana na kueleza historia ya taifa letu kabla na baada ya uhuru na sio kwa familia ya Kahama tu,”alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo mwandishi wa kitabu hiko Joseph Kahama alisema kuwa kitabu hiko kinachambua mahusiano ya kiuchumi baina ya Tanzania na nchi rafiki hususani Jamhuri ya watu wa China.
“Imani yangu baada ya kuwa karibu na China na kuelewa mifumo yao ya kiuchumi na matumizi ya rasilimali katika kukuza uchumi, Tanzania inaweza kufikia hali ya uchumi wa nchi ya maendeleo ya kati,”alisema.
Hata hivyo balozi George Kahama alikiri kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo akiwa mtumishi alishindwa kuyafanikisha, aliyataja mambo hayo kuwa ni ujenzi wa makao makuu ya taifa Dodoma.
Pili ni kuanzishwa kwa benki ya ushirika alisema akiwa waziri wa Ushirika na Masoko 2000-2005, alidhamiria kuanzisha benki ya ushirika ambayo ingeshirikisha Saccos zote nchini kama wanahisa wakuu.
Mwisho ni ndoto ya Zanzibar akiwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa hoteli za serikali ya Zanzibar, alifahamu vizuri mandhari na utajiri wa Zanzibar ambao ukitumiwa vizuri unaweza kuinua uchumi wa Tanzania na kuitangaza vyema sekta ya utalii nchini..Imeandikwa na UMMY MUYA. SOURCE: MWANANCHI.

Skuli bila ya madawati


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mateves iliyopo wilayani Arusha mkoani Arusha wakifanya mtihani wa majaribio wa nusu ya mwaka wakati wengine wakiwa wameketi chini kutokana na upungufuwa madarasa . Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 910 ambao wanatumia madawati 320 tuuu katika madarasa hayo sasa hebu nambie upungufu uliopo. Piga picha hapo unambie wanasomaje hawa watoto wa A Town. Photo by Fredy Azzah

Waziri Mkuu Pinda ziarani Vietnam


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride la heshima

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea maua kutoka kwa mtoto wa Vietnam wakati alipopokelewa rasmi kwenye viwanja vya Ikulu ya Hanoi , Machi 29, 2010 kuanza ziara yake ya kikazi nchini Vietnam. Kulia ni mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Vietnam, Nguyen Tan Dung.

Kunani Baraza la wawakilishi jamani


MWAKILISHI WA JIMBO LA MAKUNDUCHI ZANZIBAR, HAROUN SULEIMAN ALI AKICHANGIA MSWADA KWENYE UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI MJINI ZANZIBAR JANA.


MWAKILISHI WA JIMBO LA DIMANI, DK. MWINYIHAJI MAKAME MWADINI (KUSHOTO) AKIBADILISHANA MAWAZO NA MWAKILISHI WA KUTEULIWA (IKULU) ALI MZEE ALI NJE YA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI MJINI ZANZIBAR JANA.

Mpendanzoe ahamia CCJ




Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ). Picha na Tiganya Vincent-Dar es Salaam.

Vodacom yamwaga kompyuta mashuleni Singida


Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta wanafunzi wa shule ya Sekondari Isuna na ya Shelui zote za Wilaya ya Iramba,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack akiangalia jinsi kompyuta inavyofanya kazi baada ya kukabidhiwa rasmi kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za sekondari ya Shului na Isuna zote za Iramba anaeangalia kushoto Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mshamu Manyinja na Alice Mlumba.

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack(kulia)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Isuna Alice Mlumba na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Shelui Mshamu Manyinja,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.

*************************************************************************************

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 pamoja na kuunganisha mtandao wa internet kwa shule mbili za Sekondari ya Shelui na Isuna zilizoko Lindi Vijijini ili kuboresha sekta ya Elimu katika shule hizo.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Meneja wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule alisema kwamba msaada huo ni mwendelezo wa awamu ya tatu ya Mradi wa Ugawahi kompyuta kwa shule za sekondari za vijijini. Katika awamu ya kwanza na ya pili jumla ya shule 30 kutoka mikoa tofauti 15 zilifaidika katika mradi huu.

Alisema huu ni mwanzo tu kwani Vodacom Foundation itaendelea kutoa misaada ya kompyuta katika shule za mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa unalenga kutoa wimbi la uduni wa Teknologia ya kompyuta na kuinua elimu na kuisaidia serikali kama sekta binafsi siyo kuiachia serikali pekee lazima tuwe pamoja kuendeleza misingi iliyobora ya elimu.

Naye Mkuu wa Wilaya, akipokea msaada huo aliishukuru kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake huo na kusema sera ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa misaada mbalimbali ya kuiokoa jamii kama Vodacom ni mfano wa kuigwa na mashirika mbalimbali ili waweze kuisaidia serikali na wananchi wanaopatwa na upungufu wa vitu muhimu katika jamii.

“Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba uwekezaji una kua na wawekezaji pia wanapata fursa ya kuchangia maendeleo ya sekta ya kijamii nchini’

Alisema hivi sasa bila teknolojia ya kisasa amna maendeleo na alichukua frusa hiyo ya kuwaasa wanafunzi wazitunze kompyuta hizo na kuzitumia vizuri kwani mpo sambamba na shule zailizoko mjini sasa.

JK apokea misaada toka China


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam leo asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepanda katika pikpiki aliyokabidhiwa na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xingshen kama seshemu ya msaada wa China kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Misaada mingine iliyokabidhiwa katika hafkla hiyo ni pamoja na baiskeli, chupa za maji na mashine za kushonea nguo.

Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro.

Too much blessing that has turned in to agony



As you step into her one and only living cum bed room at Ukonga Mombasa in Dar es Salaam, you are welcomed by the cries of the babies.
Sophia Salum, a 28 year old mother of two, who on giving birth to the third child, she delivered triplets at Muhimbili Hospital, taking her number of children to five.
When we paid her a visit with a colleague the two were laying on bed while Sophia was bottle feeding one. They all were in white sweaters and orange slim hem.
Currently they live in a small room where they also shelter their children. And come nights, they have a small bed, which though not big enough, they sleep together, the couple, the triplets and the two other children.
It’s quite unimaginable how things can take a twist, despite our anticipations. That’s exactly how she describes the situation.
Sophia was shocked after getting the news she had delivered three children because no one in their family had ever delivered triplets.

Even though, the mother of five admitted her family has a history of delivering twins.

After delivering three children at ago, Sophia faces challenges in breastfeeding as she says s she doesn’t get enough balanced food diet to help her to produce milk for her babies. But the poverty is haunting them, making it literary impossible Sophia and her husband, Ustaadh Mohammed Wachala.

“Because of that problem we decided to buy them Lactogen in order to make them milk, most of the time her husband earned money through begging, but there is time when we fail even to get a cent to buy them a milk so what we do is prepare for them light porridge” Sophia, whose triplets are now one month and twelve days old, says.

There was a moment, she recalls, when her husband had to sell his mobile phone at a throw away price just to buy lactogen for their children. On average, 2 lactogens last for two days.
“some days she eats only a single meal a day, and that meal turnes out to be Ugali with dagaa or Okra, how do you expect her to be able to produce enough milk to breastfeed the children if she can’t get balanced diet?,” Queries her husband, who is jobless.

While there have been reports that many women with triplets pregnancy often go through difficulties during delivery processes and some of them end up dying or losing their infants, she thanks God that both she and her three babies are surviving.

She remembers they had an appointment with the doctor for Caesarian/operation after being told that her life was in danger.

“Thanks to doctors and nurses at Muhimbili hospital because they operated me safely and I didn’t pay anything”says Sophia
“I didn't believe it at first.” She says because she just couldn't understand how it was possible. She believes her triplet pregnancy is a 'gift from God'.

Ustaadh Mohammed Wachala is Sophia's husband, he looks healthier than her wife despite being jobless Despite the difficulties that came long with having to contend to keep triplets with meager finances they have, it’s a blessing in disguise the husband says.
“Though it is difficult to raise them, I am happy for this is a three ties reward. How many people outside there are crying for not being able to get babies? What I know is that every child comes along with his fair share of blessings from God” the husband says.

Support from family
Emotionally, the new mothers may constantly feel uncertain, anxious, and lack self-confidence in coping with more than one baby. It is during this time that emotional support from her spouse and family members is most important.
“We didn’t want to ask help from the people out there, we had banked our hopes on our families knowing they wouldn’t fail us come what may. But it seems they are not able to do it anymore,” she says
She said that the two families, hers and her husband's helped them however they could ,but she thanks her sister Husna who is there to cook and take care of the whole family.

“My husband is a carpenter by proffessional, and ever since he lost his job, he’s been searching for one unsuccessfully for a very long time in vain,” said the wife, adding that, prior to deliver, she was herself selling roasted cassava in street
“And I think our families have other responsibilities so it is hard to keep on persisting to ask for their support.” However she still thank her younger sister Husna Salum who is there to help her out with taking care of the kids.
Call for help
For Sophia, the future and her children’s life fate is seen in capital. She is calling for well wishers, government and various organizations to help them with capital so that they start a business of their own and stop living on aid from people daily. “That way we’ll be able to generate our own income and raise our five kids happily.” says Sophia whose health looks weaker and her lips look dry too.
Her husband is still search for help to social services though he seems tired of being asked of coming tomorrow. Story by By Elizabeth Tungaraza.

Sunday, March 28, 2010

Chadema wamzika Balozi Ngaiza


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa mmoja wa wadhamini wa chama hicho, marehemu Balozi Christopher Ngaiza, kbala ya mazishi yake yaliyofanyika
nyumbani kwake katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba mkoani Kagera jana. (Picha na Joseph Senga)

Mbunge Lucy Kiwelu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salama za mwisho kwa mwili wa marehemu Balozi Christopher Ngaiza, ambaye alikuwa mdhamini wa chama hicho, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani
kwake katika kijiji cha Mbale wilayani Muleba mkoani Kagera jana. (Picha na Joseph Senga)

Sir George enzi hizo


SIR George akiwa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julius Kambarage Nyerere katika moja ya vikao vyao mara baada ya taifa kupata uhuru, kushoto kwa mwalimu ni Rashid Mfaume Kawawa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa wakati huo na anayefuata ni Paul Bomani aliyekuwa Waziri katikaserikali ya awamu ya kwanza, wote watatu sasa ni Marehemu isipokuwa Sir George. Maktaba.

CC yakutana leo


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine katika picha ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume, Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba, Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa, Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa na Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha. (photos by Freddy Maro).

Chinga kila kona nchini


Si jambo la Kawaida kumuona mwanadada akifanya biashara ya kutembeza bidhaa za Nguo maarufu kama ‘Umachinga’, lakini mjini Dodoma utaweza kukutana nao kama alivyokutwa dada huyo na mpiga picha wetu mwishoni mwa wiki. Picha na Jube Tranquilino

Spika Sitta ndani ya Bangkok




Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta, akifuatilia kwa makini ufunguzi rasmi wa mkutano wa 122 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ulioanza rasmi jana mjini Bangkok, Thailand kwa kufunguliwa na Mtoto wa Mfalme wa nchi hiyo, Princess Maha Chakri Sirindhorn . Walioketi kusho ni balozi wa Tanzania nchini Malaysia anayesimamia pia Thailand, Mhe. Cisco Mtiro, Mhe, Dkt Christine Ishengoma, Mhe. Idris Mtulia na Mhe. Suzan Lyimo. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge. Juu Spika Sitta akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wenzake aliiongozana nao katika msafara huo.

Saturday, March 27, 2010

JKazindua ujenzi wa machinjio ya kisasa


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi Dr.John Pombe Magufuli(wapili kushoto),Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange(wanne kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za taifa Bwana Salum Shamte(kushoto) muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika machinjio ya kisasa huko ruvu mkoa wa Pwani unaofanywa na shirika kla SUMA JKT leo asubuhi.

Wataalamu wa ujenzi kutoka katika shirika la SUMA JKT wakimpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa unaofanywa na shirika hilo wakati Rais alipokuwa akikagua ujenzi huo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika machinjio hayo leo asubuhi.
(Picha na Fredy Maro)

Ajali ya Kibamba yaua familia moja


AJALI ya lori na basi dogo iliyotokea juzi Kibamba, Dar es Salaam iliua watu wawili wa familia moja akiwamo mjamzito na kusababisha mtoto mwingine kubaki yatima, imebainika.

Waliokufa ni mjamzito na mumewe ambaye alikuwa akimsindikiza mkewe siku hiyo kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhudhuria kliniki.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu wa kiume, Issa Ngoro, kaka yake kwa jina la Ibrahim Hussein Ngoro na mkewe Zainab Ali aliyekuwa na ujauzito wa miezi minane ndio waliokumbwa na janga hilo.

Issa alisema kaka yake alikuwa mfanyakazi katika bandari ya Dar es Salaam na alikuwa na kawaida ya kudamka kuwahi kazini akichelea msongamano wa magari barabarani.

“Siku ya tukio, aliondoka alfajiri sana akifuatana na mkewe ili ampeleke kliniki Muhimbili kwanza ili kuwahi foleni ya wajawazito Muhimbili na barabarani na kisha naye awahi kazini kwake,” alisema Issa.

Alisema familia hiyo imeacha mtoto mmoja wa kike, Mwanaidi Ibrahim (4) na mimba aliyokuwa nayo ilikuwa ya uzao wa pili.

Aliongeza kuwa taarifa za ajali hiyo alizipata akiwa msikitini asubuhi, ambapo Imamu aliwatangazia kuwa kuna ajali eneo la darajani na kumlazimu kwenda kushuhudia ingawa hakuwa na uhakika kama alikuwamo ndugu yake.

“Nilipofika pale kwa kweli nilichanganyikiwa kwa jinsi maiti walivyokuwa wamekatikakatika na baada ya kuona mjamzito akitolewa, ndipo nikamwaza shemeji yangu, na baadaye kidogo nikaona mguu wa kaka ukitolewa na niliutambua kwa kuwa ulikuwa na kovu kwa nyuma,” alisema Issa.

Issa aliongeza kuwa baada ya hapo, alimpigia kaka yake simu ambayo ilikuwa haipatikani, na baadaye ikambidi arudi nyumbani huku akiogopa kumwambia mama yao na walipopiga simu ya shemeji yake ikapokewa na polisi na kuarifiwa kuwa anayepigiwa amekufa na yuko mochari.

Alisema siku moja kabla ya tukio, alikutana na kaka yake akitokea kwenye shughuli zake na alimsisitiza kukazania elimu kwa kuwa wakati mwingine alikuwa akimchangia ada na nauli ya shule.

Mdogo wa marehemu Zainab, Sharifa Ali, alisema siku moja kabla ya tukio, dada yake alimpigia simu akimweleza kuwa angekwenda kliniki na baada ya hapo angepitia kwa bibi yao Magomeni.

Alisema dada yake hakuwa na uchungu wa kujifungua na kwamba alikuwa akienda kwa ratiba za kawaida. Wawili hao walizikwa jana katika eneo hilo, katika makaburi matatu tofauti.

Katika hatua nyingine, eneo la Kibamba taarifa kuu iliyotawala midomoni mwa wakazi ilikuwa msiba huo ambapo asilimia kubwa ilikuwa ya wakazi wa pale, hali iliyowafanya kutafakari wahudhurie msiba upi.

Ajali hiyo ilisababisha vifo vya abiria wote 11 waliokuwa katika Toyota Hiace namba T615 AJW ikitokea Kibamba kwenda Ubungo ambapo iligongana na lori la mafuta ya taa aina ya IVECO Fiat namba T189 ABP na tela lake namba T192 ABP.
Hadi jana asubuhi watu watano walishatambuliwa.Imeandikwa na Lucy Lyatuu; SOURCE:HABARI LEO

Jk azindua kitabua cha historia ya harakati za Sir George


JK akiwa katika picha ya pamoja na Joseph Kahama(Wanne kushoto) ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu maisha ya mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jijini Dar. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamim Mkapa, Sir Geroge Kahama(wapili kushoto) na kulia ni Rais Mstaafyu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

JK akikata akizindua kitabu kinachohusu historia ya maisha ya utumishi serikalini ya Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kutoka kushoto waoshuhudia uzinduzi huo ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama(wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi(wanne kushoto) na watano kushoto ni Mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Royalty Bwana Joseph kahama

Friday, March 26, 2010

Mamia ya miti yapandikizwa Dar




Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi (kushoto) akipanda mti kuazimisha siku ya utunzaji wa mazingira jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeendeshwa na Shirika la linalojishugulisha na shuguli za utunzaji wa mazingira na mimea la WWF kwa kushirikiana na Zain Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta.

======================================

MAMIA ya miti imepandwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam katika zoezi lililofanywa na kampuni ya simu za mikononi nchini Zain Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Mazingira na Mali hai zingine (WWF) pamoja na Manispaa ya Kinondoni jana walishiriki kazi ya upandaji miti, ili kushiriki saa moja ya kuzima taa katika miji mikubwa duniani.

Saa moja ya kuzima taa huadhimishwa Machi 27 ya kila mwaka kwa nia ya kuonyesha umuhimu wa kupunguza hewa ya ukaa na uhifadhi wa mazingira na kutoa elimu juu ya athari ya uharibifu wa mazingira kwa binadamu.

“Kampeni hii ilianza rasmi mwaka 2007 nchini Australia hadi sasa ikiwa inatarajia kupata nchi washiriki zaidi ya 120 ukilinganisha na miji 88 iliyonga mkono suala hili hapo awali;

“Zoezi hili huenda sambamba na kuzima taa kwa muda wa saa nzima kuanzia saa 2.30 usiku tarehe 27 kila mwaka, hufanya hivi kwenye Miji mikubwa ili kuwakumbusha kuwa uhifadhi wa mazingira ni muhimu na kuna haja ya kupunguza joto duniani,”alisema Meneja uhifadhi wa WWF Tanzania Petro Masolwa.

Aliongeza kuwa, kulingana na hali halisi ya umeme Tanzania kuwa ya matatizo wao wameamua kufanya zoezi la upandaji miti badala ya kuzima taa, ili kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza mazingira.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khaled Muhtadi alisema, wadau wa mazingira walioshiriki wameonyesha kuguswa na suala hilo na kuahidi kutoa ushirikiano pamoja na kampuni yake katika kutunza mazingira nchini.

“Tunafurahi kushiriki katika mradi huu, tunawashukuru wadau wa mazingira,Manispaa ya Kidondoni na WWF kuweza kufanya zoezi hili, tutatoa ushirikiano wa karibu ili kutunza mazingira,”alisema Muhtadi.

Mkuu wa Wilaya Kinondoni Jordan Rugimbana aliyasihi makampuni mengine kuiga mfano huo ili kuinusuru nchi kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Kuna haja ya makampuni mengine kuiga mfano huo matokeo ya mafuriko kama yaliyoleta maafa Kilosa na ukame maeneo ya Loriondo ni mabadiliko yenye kuhitaji jitihada za maksudi kuchukuliwa ili kuinusuru nchi yetu,”alisema Rugimbana.

Miti hiyo aina ya Washington Palm ilipandwa katika manispaa ya Kinondoni kuanzia Moroko Mataa hadi Namanga, zoezi hilo likitarajiwa kuendelea katika sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam na nchi nzima. Imeandikwa na Aziza Athuman. SOURCE: MWANANCHI

Thursday, March 25, 2010

Ajali mbaya sana





Wananchi wakiwa wanaangalia ajali ya lori ainaya scania lenye namba za usajili T 169 ABF ambalo lilipata ajali baada ya kuligonga na kuliangukia toyaota Hiace yenye namba za usajili T615 AJW lililokuwalikotokea kibamab kuelekea Jijini Dar es Salaam,ambapo inasadikiwa watu zaidi ya kumi walikufa papo hapo.

Lori la mafuta likiwa linavutwa ilikiuweza kuondoa maiti ambazo zilkuwa zimelaliwa katika ajali hiyo

Lori likiwa linavutwa baada ya kupata ajli eneo la darajani Kibamba lenye nambari za usajli T 169 ABF (Picha zote na Sanjito Msafiri)

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&


TATIZO la kutokuwepo kwa vifaa vya ukoaji hapa nchini limeendelea kusababisha vifo vingi hasa ajali zinapotokea barabarani ambapo vinapohitajika hukosekana hivyo idadi kubwa ya watu kufa eneo la tukio .

Hilo limethibitika jana katika tukio la ajali lililotokea eneo la daraja la kibamba jirani kabisa na Mji wa Kibaha ambapo lori lililokuwa na shehena ya mafuta uzito wa lita 30,000 liliigonga gari aina ya Hiace na kuilalia kwa zaidi ya masaa 5 bila ya kuwepo kwa vifaa vya aina yoyote vya uokoaji.

Akizungumza katika eneo la ajali hiyo na waandishi wa habari Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mohammed Mpinga alibainisha kuwa tatizo hilo lipo si kwa Jiji la Dar es salaam pekee bali ni la nchi nzima.

Alisema serikali kwa sasa ipo katika kuendeleza jitihada zake za uletaji wa kifaa cha uokoaji Break Down ,hata hivyo hajaweka bayana muda wa kuletwa kifaa hicho.

Ajali hiyo imehusisha lori hilo lenye namba za usajili T 189 ABD iliyokuwa na trela T 192 ABD iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Chalinze na Hiace T615 AJN iliyokuwa ikitokea Kibamba kwenda jijini Dar es salaam .

Tukio hilo limetokea majira ya saa 11 alfajiri jana na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 11 ambapo baadhi wametambulika kuwa ni Zainabu Ally ,Shukuru Hussein na Abuu Twaibu,na wengine waliotajwa kwa jina moja ambao ni Seif ambaye ni dereva wa Hiace, Bweto na Mama Peter wote wakiwa wakazi wa kibamba.

Katika eneo hilo ajali vilio vilitawala zaidi ya masaa manne kutokana na kila aliyefika eneo hilo kuona hali halisi ya ajali hiyo iliyokuwa ya kusikitisha kwani kila maiti iliyotolewa kwenye Hiace hiyo zilikuwa nyingine zikatika vichwa na kiwiliwili,utumbo nje.

Majira ya saa 4.30 ndipo break down lenye namba T 407 BDG na T 548 BDS kutoka kampuni binafsi ya Effco Crane iliyokodishwa kwa ajili ya uokoaji iliwasili eneo hilo na kuanza jitihada za kunyanyua lori na kutoa maiti zilizokuwemo ambazo hata hivyo hazikuweza kufahamika idadi kamili kwani zingine zilisagika midhili ya nyama buchani.

Hivyo kuwa kazi ngumu hata kwa Jeshi la polisi kupata idadi kamili ya waliokufa katika ajali hiyo mbaya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ilitokea wakati fuso la mchanga ambalo namba zake hazikuweza kupatikana ilipotaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele na ghafla lilipoona gari jingine lilirudi katika sehemu ya awali hivyo lori kutaka kuigonga fuso na hivyo kutoka upande wa pili na kukutana na hiace na kuiburuza na kuzama nayo mtaroni na kusababisha ajali hiyo.

Polisi kutoka Dar es salaam waliweza kudhibiti hali ya usalama katika eneo la tukio ,kudhibiti wizi kutotokea,uhamishaji wa mafuta katika lori jingine kwa ajili ya kuepusha kulipa kwa moto kutokana na gari hilo kuwa na mafuta .

Hata hivyo polisi imesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao madereva wengi hupelekea matatizo kama hayo kutokea,

Dereva wa lori ambaye anadaiwa kusababisha ajali hiyo amekimbia baada ya tukio na hadi sasa hajaweza kupatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Taarifa ya Julieth Ngarabali, Kibamba.

Wednesday, March 24, 2010

Usafiri Dar es Salaam



Unaweza kufikiri kuwa tatizo la usafiri katika nchi yetu limepungua lakini halitaisha leo wala kesho hebu angalia hapa jiutihada zinazofanyika zimewezesha angalau watu wenye magari makubwa kama hivi kupunguza msongamano wa abiria lakini bado inatakiwa kuanzisha mabasi ambayo yatakuwa na jukumu la kuwabeba abiria wakati wa kwenda kazini na kurudi ili kupunguza msongamano wa vijiggari vingi barabarani.

Operesheni Sangara





Wakazi wa Kibaigwa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakimlaki Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kabla ya kuhutubia mkutano wa juzi, ikiwa ni sehemu ya ‘Operesheni Sangara’ inayoendelea mkoani humo. Picha na Jube Tranquilino.

habari ndo hiyo

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, Ephraim Mafuru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wa HabariLeo na Daily News wakati Vodacom alipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo kutangaza rasmi pungozo la gharama za upigaji simu. Kushoto ni Mhariri Msaidizi wa Daily News, Gabby Mgaya na kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom, Mwamvita Makamba.Punguzo hilo la gharama za upigaji siku linakwenda kwajina la HABARI NDIO HIYO.


Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd na kulia ni Mkurugenzi wa Mkuu wa Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba wakizindua rasmi “habari ndiyo hii”kwa wateja wa mtandao wa Vodacom ambapo mtandao huo umeshusha gharama za maongezi kwa wateja wake kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...