Wednesday, July 30, 2008

Ze Comedy mambo bado


Pichani ni Kundi la Ze comedy wakishagilia kwa pamoja muda mfupi baada ya
Mahakama kuu kutupilia mbali ombi la EATV dhidi ya kikundi hicho..
--------
Na Emmanuel Mrema.
Mahakama Kuu,Kitengo cha Biashara imetupilia mbali pingamizi ya kituo cha televisheni cha EATV dhidi ya kikundi cha wachekeshaji cha Ze Comedy.Akisoma uamuzi huo,Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Catherine Urio alisema pingamizi tatu zilizotolewa na EATV dhidi ya Ze Comedy hazina nguvu ya kuizuia mahakama isiendelee kuisikiliza kesi hiyo.Katika pingamizi hizo,EATV ilidai kuwa walalamikaji hawakuwa na sababu za msingi za kuwashitaki,hawakufuata taratibu za kisheria za kufungua kesi hiyo mahakamani na kwamba kiapo kilichotolewa na mshiriki mmoja kati ya wote hakijafuata taratibu za kisheria.
Jaji Urio alisema pingamizi la kwanza na la pili hajatolea uamuzi kwa kuwa unaingilia kesi ya msingi,lakini la tatu la kiapo kuna matatizo kidogo ambayo kisheria hayasumbui na kisheria inaruhusiwa waleta maombi kurekebisha kiapo hicho ili kesi iendelee kusikilizwa.
“Mahakama imeona ni vizuri warekebishe kiapo kingine ili haki itendeke kwa wote,”alisema Urio.Urio alisema mahakama itapokea maombi ya kiapo hicho kutoka kwa Ze Comedy Agosti mosi na Agosti 7 itapokea kutoka EATV ili iweze kukaa na kutolea uamuzi wake Agosti 15 mwaka huu.EATV inaongozwa na wakili wake Blandina Gogadi na Justin Kimaro wakati Ze Comedy inaongozwa na wakili Peter Swai.
Wasanii hao walikuwapo kusikiliza kesi yao ambao ni Emmanuel Mgaya‘Masanja’,Lucas Mhuvile‘Joti’Sekioni David‘Seki’,Mujuni Sylivery‘Mpoki’,Isaya Mwakilasa‘Wakuvanga’Alex Chalamila‘Mc Regan’na Joseph Shamba‘Vengu’.Kundi hilo lilikuwa likifanya maigizo katika Kituo cha EATV,lakini baada ya kumaliza mkataba wake na kuhamishia matangazo yake Televisheni ya Taifa,TBC1,limeingia katika matatizo baada ya kituo hicho kudai kuwa wao ndiyo wenye hakimiliki ya Ze Comedy.
Kundi hilo ambalo hivi karibuni lilitangaza kudhaminiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji,lilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Kitengo cha Biashara, kuishitaki EATV na pia,likidai kulipwa Sh milioni 200 kutokana na kusababisha kutofanya kazi zake.

gari lililomuua Wangwe

Chacha enzi za uhai wake baada yakunyoa rasta



Gari lililohitimisha maisha ya Chacha Wangwe Mbunge wa Tarime anayetarajiwa kuzikwa kesho likiwa limeharibika vibaya, aisee maswali sasa yapo kibao, jamaa wanadai kuwa kauawa sababu hakuwa akiendesha yeye, kalikuwa kakiendesha kaijana kanakoitwa Mallya ambako ni kanajeshi kalikohitimu huko Libya. Picha za Faraja Tranquilino wa Dodoma.

Tuesday, July 29, 2008

Bhoke Munanka

Hayati Isaac Bhoke Munanka enzi za uhai wake
Hihihiiiiii ndivyo wanavyooneana kucheka Rais Mstaafu Mkapa na Aliekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Wake wawili wa marehemu Munanka wakifarijiwa na ndugu na jamaa kabla ya kuuaga mwili wa Munanka unaozikwa jioni hii makaburi ya Kinondoni.


Ndugu na jamaa wa Marehemu Bhoke Munanka wakiomboleza kifo cha ndugu yao huyo kabla ya kuzikwa jioni hii.
Mdogo wa Marehemu Munaka akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa leo hii nyumbani kwa marehemu Munanka, Kimara Baruti.



Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohammed Abood akiwa na wambolezaji wengine leo hii nyumbani kwa Munanka, Kimara Baruti. Picha zote za mdau Kassim Mbarouk wa Mwananchi.




Waziri wa Nchi wa zamani katika baraza la kwanza la mawaziri wa Serikali ya awamu ya kwanza Mh. Isaac Bhoke Munanka aliyefariki dunia Jumamosi ilopita akiwa na umri wa miaka 81 anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni, Dar.
Matanga yapo nyumbani kwa marehem huko nyumbani kwake Kimara, Dar.
kwa habari zaidi bofya hapa

Sunday, July 27, 2008

Sports day kwa mamiss



Baadhi washiriki wa shindano la Vodacom  miss Tanzania 2008   
wakicheza soka ya ufukweni wa South Beach Hotel, iliyoko Mjimwema Kigamboni Dar es Salaam, kuadhimisha siku yao ya michezo .

Jengo la kale Hatariii!!!


Mtoto wa mtaa wa Mwambao Bagamoyo , akicheza karibu na ukuta wa jengo linalodaiwa kujengwa mwaka 1830, majengo mengi ya kale ambayo yangetakiwa kuhifadhiwa na kuwa kumbuklumbu yameachwa na uongozi wa mji huo kuanguka ni hatari kwa utalii wa mji huo. Picha ya Mdau Deus Mhagale.

Mechi ya Wabunge



Kipa wa Bunge, Iddi Azan na mbunge wa Kinondoni pamoja na mlinzi wa Bunge Mzee Ngwali Zuberi ambaye ni mbunge wa Mkwajuni wakiokoa mpira wa hatari katika mechi kati ya Bunge na CRDB iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma Julai 26,2008. Bunge ilishinda 1-0. Kushoto ni mlinzi wa Bunge na Mbunge wa Sengerema William Ngereja na kulia ni mshambuliaji wa CRDB, Godwin Semunyu.


Mlinzi wa Bunge, Mzee Ngwali Zuberi(kushoto) ambaye ni mbunge wa Mkwajuni akichuana na mshambuliaji wa CRDB, Godwin Semunyukatika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Julai 26,2008. Bunge ilishinda 1-0. (Picha zote na Ofisi ya Waziri mkuu)

Akudo Sound jana



Wacheza shoo wa kundi la Akudo Impact wakisakata sebene wakati wa onesho la kutimiza miaka mitano ya bia ya Serengeti
lililofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Picha na Jube Tranquilino

Friday, July 25, 2008

usafiri bongo


Kwa hakika usafiri wa mijini una mambo yake hebu mcheki huyu mshikaji na hilo zigo japo ni zigo la sponji lakini bado kuna matata mengi dhidi yake kwanza haoni nyuma, zigo limemzidi kimo na linayumbayumba, lakini ndiyo hivyo mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe.

Citizen editor scoops top CNN award


alt=""id="BLOGGER_PHOTO_ID_5226822159520353330" />
Citizen editor Richard Mgamba (left) acceps the CNN/Multichoice African Journalist of the Year Award for the print general news category in Accra on Saturday.Below is the story that landed Mr Mgamba the honour as published by Sunday Citizen last year.

The Citizen's News Editor, Mr Richard Mgamba, has won this year's CNN Multichoice Africa Journalist of the year award in the print news category.

He was named the winner of the prestigious award at a gala awards ceremony held in Accra, Ghana on Saturday. Ghanaian President John Kufour attended the ceremony in The State Banquet Hall.

Mr Mgamba has been honoured for his coverage of the fate of small-scale miners at the Buzwagi Gold mines in Western Tanzania.

The miners were evicted from the mining area early last year to pave way for a Sh520 billion ($400 million) project by a foreign investor.

His recognition becomes the third for a Tanzanian journalist in the 13-year history of the awards. Other journalists who previously won the awards in different categories are Ms Betty Mkwasa and former Sunday Citizen Editor Sakina Datoo in 2002 and 2004, respectively.

Ms Mkwasa was then with ITV as a senior news anchor. She is now the District Commissioner for Korogwe.

In this year's finals, Zimbabwean journalist Hopewell
Rugoho-Chinono scooped the overall winner's award. The competition received 1912 entries from 44 countries throughout the continent, including French and Portuguese speaking Africa. There were 23 finalists from 14 countries.

Tears of joy overcame Mr Mgamba after receiving his trophy. "I dedicate this award to the small-scale miners who suffered at the expense of multinational companies," he said. By Erick Kabendera, Accra.

Thursday, July 24, 2008

TID afungwa jela mwaka mmoja


Picha juu msaniii TID akitoka kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Muda Mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo cha Mwaka Mmoja Leo..
-----------
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela msanii wa muziki wa kizazi kipya,Bongo Fleva,Khalid Mohammed 'TID' baada ya kutiwa hatiani kwa kujeruhi. TID,26,mkazi wa Kinondoni Hananasif,Dar es Salaam alitiwa hatiani jana katika mahakama hiyo iliyokuwa imefurika watu mbalimbali,wakiwamo ndugu wa msanii huyo, wazazi na baadhi ya marafiki zake,wote wakitaka kujua hatima ya msanii huyo.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo,Hamisa Kalombola kabla ya kutoa hukumu hiyo alisema kwamba kesi hiyo,kwa upande wa mlalalamikaji ilikuwa na mashahidi wanne na ushahidi waliota mahakamani, umeonyesha wazi kuwa msanii huyo alitenda kosa hilo.

Hakimu Kalombola aliendelea kusema kuwa,kulingana naushahidi uliotolewa umeonyesha wazi mtuhumiwa alitenda kosa kwa makusudi,hivyo kuishawishi mahakama kumtia hatiani.
Kwa upande wa mshtakiwa hakuwa na shahidi,kwani shahidi aliyepaswa kutoa ushahidi alielezwa kuwa alikuwa ni rafiki yake wa kike ambaye alikuwepo katika tukio,lakini ilielezwa mahakamani hapo kuwa alikuwa safari na hivyo kumsababisha rafikie kukosa shahidi.

Kabla ya kutoa hukumu,mahakamani hapo,Hakimu Kalombola alisoma maelezo ya awali ambako ilidaiwa kuwa Julai 2 mwaka jana saa 6:30 usiku katika Hoteli ya Slipway,eneo la Masaki wakiwa katika ukumbi wa burudani,mtuhumiwa alimpiga mlalamikaji Ben Mashibe kwa kutumia trei la chupa za bia na kumsababishia maumivu makali.
Ilidaiwa kuwa kitu kilichomsabisha msanii huyo kuanzisha fujo ni kutokana na begi alilokuwa ameshika rafiki wake huyo wa kike,kutoonekana kwa muda huo,hivyo kusababisha watu waliokuwapo mahali pale ikiwa ni pamoja na mlalamikaji kuanza kushambuliwa.
Baada ya kusoma maelezo,Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea,ambako alisema kwamba alikuwa amepitiwa siku ya tukio kutokana na pombe alizokuwa amekunywa,hivyo akaiomba mahakama iahirishe kutoa hukumu hiyo.

Mtuhumiwa alijitetea kuwa anayo familia inayomtegemea katika kuwalea, isitoshe mama yake mzazi hana kazi, naye pia anamtegemea kwa kila kitu.Kwa upande wake,Mwendesha Mashtaka, Inspekta wa Polisi,Benedict Nyagabona alidai kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani umeithibitishia kuwa mtuhumiwa alitenda kosa,hivyo anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Inspekta Nyagabona alidai kuwa kuwa kitendo cha mtuhumiwa kunywa pombe kupita kiasi hadi kuwasababishia watu madhara,ni kinyume na sheria,hivyo anatakiwa apewe adhabu kali kwa kuvunja sheria na pia kuleta madhara kwa jamii.Hata hivyo,wakati akiondolewa mahakamani hapo,msanii huyo alionyesha dhahiri uso wa majonzi huku ndugu zake nao wakionyesha kufadhaika.

Kabla ya kupanda karandinga,TID alikabidhi mali zake ikiwamo simu ya mkononi kwa mtu ambaye alidaiwa ni msanii mwenzake,ambaye hata hivyo alisikika akimweleza asikate tamaa ya maisha,ataweza kumaliza kifungo chake.Habari hii kwa msaada wa Elizabeth Suleyman.Picha na Mdau Msimbe.

Wednesday, July 23, 2008

Nani kutwaa taji la Vidacom Miss Tanzania 2008


Florence Josephat kutoka Kanda ya Temeke


Nadya Ahmed kutoka kanda ya Kaskazini-Tanga
Picha mwanana za Vimwana(Tausi)wanaoshiriki shindano la kutafuta Miss Tanzania 2008 wakiwa katika pozi mbalimbali kambini kwao leo mjini bagamoyo ndani ya Paradise Beach Resort ambapo kwa leo ilikuwa ni siku malum kwa vyombo mbalimbali vya habari kukutana na vimwana hivyo.

Tuesday, July 22, 2008

Migiro ndani ya bongo


Mbunge wa Same Mashariki Anne KilangoMalecela akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha-Rose Migiro hati aliyoweka sahihi kuunga mkono kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake mjini Dodoma jana. Pichana Jube Tranquilino

nishati mgogoro


Nishati ni tatizo kubwa saana bongo, wengine wanatumia mavi ya ng'ombe kama nishati, wenye uwezo kiasi au sana wanatumia umeme, baadhi wanajitahidi kutumia gesi ili mradi kila kitu vurugu tupu, pichani kina mama wa kibongo wamebeba kuni tayari kwa matumizi ya nyumbani. Unasemaje ndugu msomaji hapa wewe unatumia nishati gani mbadala ya hii je, ni upepo au ni nini???, na je hizi ni kuni au ni vijiti????

Mizengwe dhidi ya Dk Masau



MWANZILISHI na Rais wa Hospitali ya Taaisi ya Moyo Nchini (THI) Dk Ferdinand Masau amegoma kuhama katika jengo la Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambako anaendesha shughuli zake.

Dk Masau alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa mkutano wa VC uliopo ndani ya Jengo la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina ya madaktari wa moyo.

Dk Masau alisema hawezi kuhama katika jengo hilo kwa sababu NSSF imeshindwa kutimiza makubaliano yao wakati walipompangisha na kwamba kuna wagonjwa pamoja na mali za THI.

“Kwanza siwezi kuhama katika jengo hilo kwasababu kuna wagonjwa 15 wamelazwa ambapo kati yao wagonjwa 5 wanategemea kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati wowote, pili vitu ambavyo viko ndani ya jengo hilo ni zaidi ya bilioni, makubaliano yetu ilikuwa ni kutengeneza jengo hilo ili liwe na hadhi ya hospitali ya moyo kitu ambacho walishindwa kuyatimiza ,”alisema Dk Masau.

Alisema moja ya makubaliano yao ni kwamba NSSF wamtengenezee jengo liwe na hadhi ya Hospitali ya Moyo.

Alisema baada ya makubaliano hayo NSSF walimpelekea taarifa kuwa kazi hiyo imeshamalizika hivyo anachotakiwa kufanya ni kukubali kusaini mkataba wa kulipangisha jengo hilo.

“Nilikubali kusaini mkataba wa kama mpangaji baada ya NSSF kunihakikishia kuwa wamenitengenezea jengo hilo kama nilivyowaeleza, lakini baada ya kusaini mkataba na kuingia ndani ya jengo nikagundua kuwa kuna baadhi ya maeneo hayajatengenezwa kama nilivyoyahitaji,”alisema Masau na kuongeza:

“Baada ya kubaini mapungufu hayo tulikubaliana niendelee kulitumia jengo hilo wakati marekebisho hayo yanafanyika, lakini hayo hayakufanyika badala yake nilishangaa kuona taarifa ya kuitwa mahakamani kwa kesi ya madai miezi miwili baada ya mkataba huyo,”alisema.

Alifafanua kuwa baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa mahakamani miezi miwili baadaye hukumu ilitolewa na mahakama ikaamuru aondolewe katika jengo hilo na kwama baada ya amri hiyo alimfuata Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambapo Waziri aliwataka wayamalize nje ya mahakama chini ya Wizara ya Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Uamuzi wa kumuondoa katika jengo hilo lilitolewa jana na Shirika hilo katika vyombo vya habari iliyokuwa na kichwa cha habari ilisomeka kama taarifa kwa umma akidaiwa kushindwa kulipa deni la jengo hilo lenye thamani ya Sh 2.3 bilioni.

Sehemu ya taarifa hiyo ilisema kuwa NSSF inatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa, kwa muujibu wa amri ya Mahakama Kuu (kitengo cha Ardhi) iliyotolewa Septemba 11 mwaka jana katika shauri na 158/2007 kati ya NSSF na Taasisi ya moyo Tanzania.

“NSSF itatwaa jengo lake lililojulikana kama”Hosteli ya Tazara” ambapo kwa sasa limepangishwa na THI Julai 25 mwaka huu hivyo wagonjwa wote na familia zao wanashauriwa kufanya mpango mbadala ya hospitali ya kuhama au kuhamisha wagonjwa wao kabla ya tarehe hiyo kufika,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, kufuatia taarifa za ndani ya NSSF zilizonaswa na Mwananchi zimebaini serikali ilishawahi kutoa tamko kuwa haiwezi kingilia zaidi mgogoro huo na kuwataka wamalize mgogoro huo kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo za siri pia ilibaini kuwa Julai 5, Waziri wa Kazi Ajiri na Maendeleo ya Vijana Profesa Juma Kapuya alimuandikia Dk Masau barua iliyosema kuwa endapo atashindwa kulipa sehemu ya deni hilo kama walivyokubaliana katika kikao cha Julai Mosi mwaka huu NSSF itaendelea na uamuzi wake wa kumtoa ndani ya jengo hilo.

“Tulikubaliana kuwa endapo taasisi yako itashindwa kulipa sehemu ya deni hilo kama inavyopendekezwa basi NSSF itaendelea na uamuzi wake wa kuitoa hiyo THI kwenye jengo hilo kama iliyoamuriwa na mahakama bila kutoa notisi nyingine,”ilisema sehemu ya barua hiyo ya Waziri Kapuya.

Hata hivyo, nakala ya barua ilipelekwa kwa Waziri Mkuu,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na NSSF. Habari na Jackson Odoyo na Saida Amini

Dk Migiro ndani ya bongo


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose-Migiro, akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mlimani Dar es Salaam jana, alipohudhulia sherehe za kukabidhana maktaba ndogo ndogo za kisasa zilizogengwa katika mikoa ya pweani na Dar es Salaam chini ya mradi maalumu wa Mmoja wa Mataifa wa (UNWTO Step Foundation). Picha na Emmanuel Herman

Sunday, July 20, 2008

Zimbabwe yaanzisha noti ya bilioni 100



BENKI Kuu ya nchini Zimbabwe imeingiza katika mzunguko noti za dola ya Zimbabwe bilioni 100 . Januari mwaka huu Zimbabwe iliingiza katika mzunguko dola ya Zimbabwe milioni 10.
Nia ya kuingizwa katika noti hiyo katika mzunguko kunatokana na kuzidi kukjosekana kwa fedha kunakotokana na kuzidi kwa mfumuko wa bei.
Pamoja na kuonekana kuwa nyingi, fedha hizo hazitoshi mkate.Kiasi cha mfumuko wa bei kwa sasa ni asilimia 2,200,000.Wataalamu wanasema kiwango cha mfumuko ni zaidi na huo unaoelezwa na Zimbabwe. Asilimia 80 ya wananchi wa Zimbabwe kwa sasa wanaishi katika umaskini mtupu.
Januari mwaka huu Zimbabwe ilitoa noti ya dola milioni 10 na kufuatiwa na dola milioni 50. Hebu soma
cheki BBC



Elimu kweli safari yake ndefu


Zuena Yahya, akimvisha shada la maua Salma Taituz, baada ya kuhitimu shule ya awali ya St Mary's Mbagala jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo juzi. Picha ya Deus Mhagale.

My God wamegonga gari langu


Dereva aliyekuwa akiendesha gari la Ubalozi wa China nchini, akiwasiliana na ubalozi wake baada ya gari lake kugongana na gari dogo aina ya Toyota Starlet ambayo ilikimbia baada ya kusababisha ajali hiyo, makutano ya barabara za Kawawa na Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam juzi. Picha ya mdau Kassim Mbarouk.

Safari ya Rais Tanga

Rais Jakaya Kikwete, akimsikiliza yatima aliyekuwa akimwomba msaada wa kuweza kujikimu mara baada ya kuzindua kiwanda cha Gesi Mkonge na Umeme Mkonge iliyofanyika Hale mkoa wa Tanga hivi karibuni, kuli ni Felix Francis wa shule ya msingi Unyanyembe ya Hale.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari za Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga, wakishangilia kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete kuanza ziara ya siku moja katika wilaya hiyo majuzi. Picha zote za mdau Deus Mhagale.

Friday, July 18, 2008

Maskini Esther Katua


MWANDISHI wa habari wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Esther Katua (pichani), amefariki dunia.

Esther alifariki katika hospitali ya Lugalo Dar es Salaam jana, alikokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya.

Alifikishwa hospitalini hapo Jumatatu ya wiki hii baada ya kuzidiwa alipokuwa
akijiuguza nyumbani kwao Ilala, Dar es Salaam.

Kifo cha mwanahabari huyo kimetokea siku ambayo pia alichaguliwa kuwa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tawi la Uhuru na mjumbe wa UWT wa tawi kuwakilisha vijana.

Wakati wa uhai wake, mbali ya magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Esther aliwahi
kuandikia magazeti ya ZanzibarLeo na Mwananchi. Esther alijiunga na magazeti ya Uhuru katikati ya miaka ya 1990.

Kwa waliomfahamu Esther wakati wa uhai wake, alikuwa ni mkarimu, mchapakazi hodari, mchangamfu na aliyependa kushirikiana na watu katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Hadi jana jioni ilikuwa haijafahamika maziko ya marehemu Esther yatafanyika lini na wapi.

BREAKING NEWS - POLISI WAVAMIA MWANAHALISI

Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa gazeti la mwanahalisi limevamiwa
muda huu na polisi huku wanaendelea na upekuzi ila hatujui wanataka nini .

Waliwakuta ofisini ndugu Kubenea Said na Ndimara Tegambwagwe pamoja na mlizi
ndugu Mayunga.

Wanaendelea na upekuzi na itakumbuka kuwa hawa hawa ndio ambao walimwagiwa
tindikali na kesi bado inaendelea japo haijulikani nini hatima ya haya mambo
Wamechukua computer ambayo anaitumia pamoja na flash na wameondoka naye
kwenda kumsachi nyumbani kwake na hili lilitokana na kuwa polisi hawa
wanatafuta nyaraka fulani Kuna amri ya mahakama ya kufanya hivyo?

Taarifa tulizo nazo ni kwamba walikuwa wakitafuta nyaraka za benki zilizomuumbua mzee wa vijisenti na kumfanya ajiuzulu hali inayowafanya waingie kiwewe labda na wao siku moja haya mambo yatawakumba.

La maana ni kuwahi mahakamani (kama inawezekana) nadhani ndio sababu wamevamia late today... lakini kama wana search warrant na kama inawapa uwezo wa kwenda kusearch hadi nyumbani.

Upekuzi nyumbani kwake unaendelea na sasa haijulikani nini kinafanyika huko kwani simu yake haipokelewi tena .

Tutawapa yaliyojiri punde.

Jengo la UVCCM liwaunguza CCM



SAKATA la utata katika mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa mwekezaji amekwisha kuanza kazi, wakati viongozi wa CCM wakidai kwamba mkataba haujasainiwa.

Wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Francis Isaac, anasema kuwa vifaa vya ujenzi vimekwisha kuwasili kwenye eneo la ujenzi kama sehemu ya matayarisho, Mwananchi imeshuhudia ujenzi halisi ukiwa umekwisha kuanza.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba licha ya juzi kusema kwamba mkataba huo haujasainiwa, jana alishindwa kueleza sababu za mwekezaji huyo kusogeza vifaa eneo la ujenzi akisema kuwa hahusiki na masuala ya ujenzi, ila mkataba ambao ameona kuwa unafaa.

Makamba aliliambia gazeti hili kuwa mkataba huo una manufaa kwa UVCCM ila hawezi kuzungumzia suala la mwekezaji huyo kusogeza vifaa kabla ya kusainiwa kwa mkataba huo kwani halimhusu.

"Mimi ninachosema mkataba huo una manufaa kwa UVCCM, kuanza ujenzi ni suala lingine ambalo mimi sihusiki nalo unaweza kuwapigia wenyewe (UVCCM) waseme kwa nini mwekezaji huyo amesogeza vifaa wakati mkataba haujasainiwa," alisema Makamba na kuongeza:

Ujenzi ni suala la kiufundi, linahitaji vibali na kuthibitishwa na mamlaka mbalimbali siwezi kuzungumzia hilo na ukitaka waulize wenyewe watoe majibu,"Habari ya Kizitto Noya

Hussein Bashe achukua fomu uenyekiti UVCCM


MWANASIASA chipukizi na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe, amejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Bashe ambaye jana alifika makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, alisema nia yake ni kuipanga upya jumuiya hiyo ili kuondokana na changamoto za kikanuni na mifumo.

"Ingawa UVCCM imejitahidi kutekeleza majukumu yake mengi kwa ufanisi, bado naona kuna changamoto nyingi, bado Jumuiya inapaswa kujipanga na kujitazama upya ili iweze kukidhi mahitaji na matarajio ya vijana wa Kitanzania kwa nyakati za sasa," alisema.

Katika waraka wake kwa wanaUVCCM, Bashe alisema akichaguliwa kushika wadhifa huo, atafanya mabadiliko ya msingi katika jumuiya hiyo ikiwamo kuifanya Jumuiya hiyo kuwa jukwaa la vijana kutoa mawazo yao.

Alisema pia atatumia fursa hiyo kubadili muundo wa utawala na kalenda ya vikao, kuanzisha kamati ya maadili, kuipa uhai idara ya chipukizi na uhamasishaji, kuifanya jumuiya kuweza kujitegemea kiuchumi na kuanzisha Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos) kwa ajili ya vijana.

Alisema pia atadhibiti uhamisho wa viongozi usio wa lazima, kuboresha maslahi yia watendaji, kuanzisha utaratibu wa kuwapatia posho wenyeviti na kuanzisha utaratibu wa kukutana na makatibu ambao ni watendaji wa chama. Habari ya Kizitto Noya na picha ya Mpoki Bukuku.

Thursday, July 17, 2008

Njia Tatu


Hii ni kali tangu yule mheshimiwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alipoingia madarakani kwa kweli hatukatai aliingia kwa nguvu kubwa akafanya mengi mno kwa muda mfupi mojawap[o ni hili la njia tatu hakika, mfumo huu umesababisha mambo mengi mabaya na mazuri, umeua watu wengi na kuwatia vilema wengine na kwamba hata bima hawatambui, sasa hivi bado tunauhitaji mfumo kama huu kwanini zisiendelee kutafutwa njia mbadala ya hii.

Sigara duuuhhh


Eeee bwana sigara sijui ni tamu au sijui vipi, ukiwaona wanaovuta huburudika saana na ladha yake wanaipata vilivyo , lakini maelezo ya kitaalamu yanasema sigara ni mbaya na inaleta balaa mwilini japo watu twaipenda, hebu mcheki mdada hapa akivuta hisia ya fegi. Picha ya mdau wa blogu hii.

Wednesday, July 16, 2008

Nauli zapaa nchi nzima



MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra), imepandisha nauli za mabasi nchini kote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra jana jijini Dar es Salaam, nauli hizo ambazo zimepanda kwa zaidi ya asilimia 20 ya nauli za awali, zitaanza kutumika rasmi Agosti Mosi, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa alisema uamuzi huo unatokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji nchini.
"Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kufikia wastani wa Sh 1,700 kwa lita ya petroli na dizeli Sh2,000, ni lazima nauli ipande na hakuna jinsi ya kuepuka hali hiyo," alisema Sekirasa.

Tume ya ghorofa yamkabidhi ripoti Kandoro


TUME iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la ghorofa kumi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Kandoro jana imekabidhi rasmi taarifa kwa mkuu huyo wa mkoa baada ya kuomba kuongezewa wiki moja zaidi na kuwa na wiki tatu badala ya mbili awali.
Tume hiyo iliundwa ili kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la ghorofa kumi lililokuwa mtaa wa Mtendeni Manispaa ya Ilala katika Kata ya Kisutu imekabidhi kazi na kukiri kwamba ilikuwa ngumu sana.
Kandoro alisema anahitaji muda wa kutosha kuipitia kwa makini taarifa hiyo na atawasiliana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na ndipo serikali itakapotoa tamko.
"Taarifa hii itachanganywa na taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza jengo la hoteli ya Chang'ombe (Chang'ombe Village) lililobomoka mwaka juzi wilaya ya Temeke na kutolewa tamko kwa pamoja," alisema Kandoro
Alisema wananchi wawe na subira kwani katika taarifa ya tume hizo hakuna kitu kitakachofichwa badala yake zitafanyiwa kazi ili kuondoa tatizo hilo na taarifa zitatolewa kwa Umma. Habarri ya Ummy Muya.

Tuesday, July 15, 2008

Masikini mama yangu


Masikini bibi yangu sijui anatapona ili anipikie uji nina njaa kwelikweli, ndivyo anavyoonekana kuwaza mtoto huyu mdogo ambaye alikutwa hivi karibuni huko temeke akimuuguza mama yake. Picha kwa hisani ya mdau wa blogu hii.
Caption sahihi : Mtoto Calvin Kika wa Tandika Temeke ambaye akimtazama kwa uchungu bibi yake Elizabeth Nyello wakati
amewekewa dripu ya kupunguza makali ya dawa juzi alizotumia dawa aina ya ldomet, Cimetidine, Amoxlin,Lasix, Metronidazole na Magnesium za kutibu B/P, kutema mate na uvimbe alizopewa hivi karibuni katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.
Picha hii ilipigwa na Zawadi Kika. Simu na mawasiliano naye naendelea kuyatafuta nitawapatieni nimepoteza kidogo.

Kipanya cha leo...

Kivumbi chaanza UVCCM



KADA wa Chama Cha Mapinduzi Nape Nnauye na mgombea uenyekiti wa UVCCM taifa, amechukua fomu leo ya kugombea uenyekiti wa umoja huo taifa.

Akizungumzia kuhusu uamuzi wake wa kugombea nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM, Nnauye alisema amelenga kukabiliana na changamoto kadhaa zinazoukabili umoja huo ikiwamo kushindwa kwake kubadilika kuendana na matakwa ya nyakati.

Alisema UVCCM ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitetea wanyonge, imeshindwa kushughulikia matatizo ya vijana kwa kukemea ufisadi jambo alilosema kuwa linahitaji kiongozi madhubuti kulifanya.

"Vijana ndio waliotembea katika Azimio la Arusha kuwafukuza mabeberu lakini leo wakati jamii inazungumzia ufisadi, UVCCM inakaa kimya!," alishangaa.

Alisema vita dhidi ya ufisadi ni ngumu na inahitaji nguvu za pamoja za vijana kupambana nayo hivyo sio sahihi kwa UVCCM yenye kazi ya kuwapika viongozi kimaadili kutoizungumzia.

Alisema mbali na changamoto hiyo UVCCM imeshindwa kuhifadhi na kutunza vyanzo vyake vya mapato pamoja na kutafuta miradi mbadala ya mapato kukabiliana na hali ngumu ya uchumi.

"... Kisiasa UVCCM imeshindwa kuweka mikakati ya kupata wanachama wapya na kudhibiti wanachama waliopo, pia imeshindwa kuhifadhi vyanzo vyake vya mapato na kwenda sambamba na mahitaji ya mabadiliko ya nyakati," alisema.

Kwa mujibu wa Nnauye UVCCM imeshindwa kubadilika na kukidhi mahitaji ya mfumo wa siasa wa vyama vingi badala yake imeendelee kung'anga'nia siasa za mfumo wa chama kimoja jambo ambalo ni hatari kwa uhai wake na chama.

"Moja ya kazi za UVCCM ni kuwa tanuru la kupika viongozi lakini hakuna mikakati yoyote ya kuongeza wanachama, kukemea ufisadi na kutengeneza vyanzo mbadala vya mapato," alisema. Habari na Kizitto Noya.

Sunday, July 13, 2008

Safari za harakaharaka za treni za Kigoma zaanza


THE Tanzania Railway Limited was yesterday launched an addition passenger train to Kigoma route.

Speaking at the ceremony, the Permanent Secretary for Ministry of Infrastructure, Eng Omar Chambo said that the additional passenger train has got 16 coaches whereas he explained that this is the effort made by TRL to make sure that it improved its services.

He said that now central railway line will have three routes a week and he added that in August this year the central railway line will have six routes a week and that TRL is aimed to easing transport problems on the central line.

Eng. Chambo said that TRL has ordered 23 coaches from India which are expected to reach in the country early in august this year the situation that will develop the central railway line routes.

He added that when the coaches arrived in the country that problem of passenger transportation within TRL will be finished since there could be enough coaches for passengers.

Meanwhile Eng. Chambo said that Tanga to Dar es Salaam railway has already started its route last month whereby cargos like cement are transported to Dar es Salaam via Tanga railway and this is the results of arrival of 25 cargo engines.
By Beldina Nyakeke, Citizen, Dar es Salaam.

Mwanza mambo tambarare




Mwanza si mchezo bwana mambo yao sasa tambarare hebu cheki hapa katikati ya jiji la Mwanza mitaa ya wapi vile suijui hebu nambie ndugu msomaji, hivi utadai kweli Mwanza eti mji mbaya, hebu cheki kuleee huioni Bugando hospital kwa mbaaali.

Maji taka kibao


Eeee bwana jiji letu la Dar es Salaam linakabiliwa na tatizo kubwa a miundombinu mibovu hali inayosababisha maji taka kutapakaa kila pahala, hebu cheki hapa stendi ya Mwenye maji taka yametapakaa kila pahala.

Miss Redds 2008





Warembo 28 wa Miss Tanzania Vodacom wakiwa katika picha ya pamoja uwanja wa ndege Mwanza baada ya kuingia Jijini Mwanza jana na ndege ya shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Leo, warembo hao watashiriki tamasha la michezo katika ukumbi wa Benki ya Tanzania (BoT) baadaye watatembelea watoto yatima na kisha Jumanne watakwenda Mara ambako watazuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Jana, walipowasili hapa walipokewa na mamia ya wakazi wa Mwanza wakiongozwa na Dk Msekela.


WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...