Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa kukabidhiwa mbegu hizo za mahindi zinazokabiliana na
ukame Wema.
Ofisa
Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila
akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Isamilo kabla ya uzinduzi wa
shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kutoka kushoto ni Mtafiti kutoka
COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo, Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku
mkoani Kagera, Jojianas Kibula, Mtafiti Bestina Daniel na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu ya mahindi.
wananchi wa Kijiji cha Isamilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkulima Hernick Elias wa Kijiji cha Isamilo akizungumzia changamoto za kilimo walizonazo
Watafiti wakifanya vipimo kabla ya uzinduzi wa shamba la mbegu za mahindi katika kijiji cha Isamilo.
Wakulima wa Kikundi cha Nguvumoja cha Kijiji cha Isamilo wakiwa shambani wakati wa uzinduzi huo.
Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Salome Renatus akizungumza na waandishi wa habari.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla ya upandaji wa mbegu za mahindi.
Ofisa Ugani wa Kijiji cha Isamilo, Issa Pegeege, akionesha jinsi ya uwekaji mbolea kabla ya kupanda mbegu ya mahindi Wema.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari (kulia), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akiongoza wakulima kupanda mbegu ya mahindi kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Isamilo.
Mkulima
wa Kijiji cha Kikundi cha Nguvu moja katika Kijiji cha Kamhanga, Hamisi
King akitoa maelekezo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mahindi
katika kijiji hicho.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla ya upandaji wa mbegu za mahindi katika Kijiji cha Isamilo.
Wakulima
na wananchi wa Kikundi cha Kasimpya katika Kijiji cha Mnekezi kilichopo
Kata ya Kaseme wakisubiri maelekezo namna ya kupanda mbegu za mahindi
katika shamba darasa.
Diwani wa Kata ya Kaseme, Andrew Kalamla akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shamba darasa hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnekezi.
Mwakilishi wa Mkoa wa Geita, Emiri Kasagala, akihutubia katika uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, Robert Gabriel
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akipanda mbegu wakati wa uzinduzi wa shamba
darasa katika Kijiji cha Mnekezi. Kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa,
Emiri Kasagala.
Na Dotto Mwaibale, Geita
MKUU
wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi amesema ataanzisha utaratibu
wa kuwapima maofisa ugani wa mkoa huo utendaji kazi wao ili kujua uwezo
wa kila mmoja wao.
Hayo
ameyasema wakati Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
ilipokuwa ikimkabidhi mbegu bora za mahindi, mihogo na viazi lishe ikiwa
ni siku yake ya kwanza kufanya kazi katika mkoa huo tangu ateuliwe na
Rais Dk.John Magufuli kushika wadhifa huo.
"Kilimo
ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika
uchumi wa kati wa viwanda hivyo nitaweka utaratibu wa kuwapima maofisa
ugani wote wa mkoa huu ili niweze kujua utendaji kazi wao" alisema
Lughumbi.
Lughumbi
aliwataka maofisa ugani mkoani humo kuacha kukaa maofisi kwenye
viyoyozi badala yake waende walipo wakulima kushirikiana nao kuwapa
elimu ya kilimo ili kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo.
Mkuu
huyo wa mkoa ameahidi kununua viatu vya shambani 'gambuti' na koti na
kuwa mara moja ataanza kutembelea wakulima katika maeneo yao ili kujua
changamoto zao na kusema anapenda kuona mkoa wa Geita unakuwa namba moja
kwa kilimo hapa nchini.
Akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu
hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH,
Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali
katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia
tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na
kuhakikisha zinawafikia walengwa.
Alisema
mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika
mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa
changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa
na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato na ukame.
Akizungumzia
mbegu bora ya viazi lishe alisema mbegu hiyo viazi vyake vinavitamini A
ya kutosha ambayo ni muhimu kwa watoto na hiyo itawasaidia baadhi yao
kuto kwenda Hospitali kuipata badala yake wataipata kwa kula viazi
hivyo.
Msangi
aliwaomba maofisa ugani pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali za
kazi yao wasisite kwenda COSTECH ili kusaidiana na kupeana mbinu
mbalimbali za kilimo.
Mkulima
wa Kijiji cha Isamilo, Hermick Elias alisema kukosekana kwa mbegu bora,
wataalamu wa kilimo na kutofikiwa na pembejeo za kilimo kwa wakati ni
moja ya sababu ambayo imewarudisha nyuma katika masuala ya kilimo lakini
wanaamini kwa mbegu hizo walizoletewa na COSTECH itakuwa nu mkombozi
kwao kwa kupata chakula na ziada watauza na kujipatia fedha za
kuwasaidia.
Alisema
kwa kilimo walichokuwa wakikifanya ekari moja walikuwa wakipata mahindi
kuanzia magunia nane hadi tisa lakini kwa maelezo ya watafiti hao wa
kilimo iwapo watatumia mbegu hiyo bora wataweza kupata magunia kuanzia
25 hadi 30.
Mkulima
Salome Renatus aliipongeza serikali na COSTECH kwa kuwapelekea mbegu
hizo hivyo wanatarajia kupata mazao yenye tija tofauti na awali.
Mbegu hizo zitapandwa katika mashamba darasa katika wilaya zote za mkoa wa Geita, Nyang'wale, Mbogwe,Chato na Bukombe.
No comments:
Post a Comment