Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa
zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Mwananyamala Bw.
Marco Sallingu kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma
ya afya jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile wa pili kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za wa
Hospitali ya Mwananyamala wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa
huduma ya afya jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa
zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Sinza Palestina
Bi. Doris Messanga kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa
huduma ya afya jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile wa katikati waliosimama akiongea na wagonjwa wakati wa ziara
yake Hospitalini Sinza Palestina alipotembelea vituo vinavyotoa huduma
ya afya jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile wa tatu kulia akiangalia nyaraka zinazoonesha jinsi ya dawa
zinavyoagizwa MSD katika Zahanati ya Mwenge wakati wa ziara yake katika
vituo vinavyotoa huduma ya afya jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile wa kwanza kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za
Zahanati ya Mwenge wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma
ya afya jijini Dar es salaam.
…………………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndungulile amefanya ziara kwenye baadhi ya vituo vitoavyo huduma za afya
kwa ajili ya kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa jijini Dar es
salaam.
Akizungumza
lengo la ziara hiyo Dkt. Ndungulile amesema kuwa ameamua kufanya hivyo
ili kuungana na Mhe. Rais wa wamau ya tano Dkt. John Pombe Magufuli
pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kutatua tatizo la dawa
katika vituo vinavyotoa huduma za afya mpaka kufikia 2020.
“Mpaka
kufikia hivi sasa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali
imetenga shilingi Bilioni 262 kwa ajili ya kutatua tatizo la uhaba wa
dawa nchini kutoka shilingi bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/2016 “
alifafanua Dkt. Ndungulile.
Aidha
Dkt. Ndungulile amesema kuwa katika ziara hiyo amegundua kwamba vituo
vinavyotoa huduma ya afya vina dawa zote muhimu isipokuwa kuna upungufu
wa vifaa tiba ambapo tatizo hilo litafanyiwa kazi mara moja .
Mbali
na hayo Dkt. Ndungulile aliwataka waganga wakuu na Wafamasia wa vituo
vinavyotoa huduma za Afya kuboresha upokeaji ,utunzaji wa dawa pindi
zinapoingia kwenye stoo zao na usimamizi mzuri wa dawa hizo.
“Vituo
vinavyotoa huduma za afya lazima ziwe na kamati za afya ambazo
zitashiriki katika kupokea dawa pindi zinapotoka MSD badala yake
zinapokelewa na mtu mmoja aidha mfamasia au mtumishi mwingine wa kitengo
cha dawa” alisema Dkt. Ndungulile.
Dkt.
Ndungulile leo amefanya ziara yake ya kutaka kujiridhisha na hali ya
upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mwananyamala,Hospitali ya Sinza
na Zahanati ya Mwenge za jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment