Mwenyekiti
wa Chama cha Makandarasi Mhandisi Lawrence Mwakyambiki (katikati)
akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) katika
utambulisho wa mkutano wa chama hicho utakaofanyika Novemba 17, 2017
Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mauzo wa benki ya
cba Bi.Kunenguda Dedede na kushoto ni Mkuu wa Masoko kutoka NMB Bi.Linda
Teggisa.
Meneja
Mauzo wa benki ya cba Bi.Kunenguda Dedede akieleza jambo kwa waandishi
wa habari( hawapo pichani) kuhusu mkutano wa makandarasi hapo novemba
17, 2017 katika ukumbi wa diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam, wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa na
Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Mhandisi Lawrence Mwakyambiki.(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Chama
cha Makandarasi (CATA) kinachounganisha wakandarasi wote nchini
kinatarajia kukutana Novemba 17, 2017 kujadili kuhusu ukuaji wa viwanda
nchini mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini
Dar es Salaam.
Akizungumuza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa
Chama hicho Mhandisi Lawrence Mwakyambiki alisema kuwa Serikali ya
Aawamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli iko kwenye
njia ya ujenzi wa viwanda kwa hiyo sekta ya ujenzi inahitajika kwa kiasi
kikubwa kwenye sera hii ya viwanda.
“Lengo
la mkutano huu kwa wakandarasi hawa ni kutaka kuleta mchango wao katika
ujenzi wa uchumi wa Tanzania na wameona kwamba kama wazawa wanaowajibu
wa kutoa mchango katika katika ujenzi wa viwanda nchini”, alisema
Mhandisi Mwakyambiki.
Aidha
Mhandisi Mwakyambiki aliseka kuwa katika maendeleo ya taifa tasnia ya
ujenzi ni muhimu kwani inabeba vitu vingi na kuwawezesha wananchi kupata
huduma stahiki kama elimu na afya na kuwataka makandarasi kufanya kazi
zo kwa ufanisi mkubwa.
Katika
mkutano huu ambapo CATA watakuwa waratibu vyama vingine vya
wakandaarasi vikiwemo Tanzania Civil Engineering Contractors
Association(TACECA) pamoja na Association of Citizen Contractors(ACCT)
na mabenki ya cba na NMB ambayo yatatoa ufadhili wa mkutano huo.
Akibainisha
miradi itakayochukua nafasi katika majadiliano hayo Mwakyambiki alisema
kuwa katika serikali hii ya awanu ya tano miradi inayohitaji
wakandarasi ni Ujenzi wa miundombinu ya reli(SGR), sekta ya maji, bomba
la kusafirisha mafuta ghafi(uganda –tanzania) pamoja na ujenzi wa makao
makuu ya nchi Dodoma.
Aidha
aliongeza kuwa katika mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuliwa na
wakandarasi zaidi ya 200 ambao watatoa mawazo yao kuelekea ujenzi
wauchumi wa viwanda kama sera ya awamu ya tano inavyoelekeza ni muhimu
kwa ujenzi wa taifa.
Mhandisi
Mwakyambiki alisema kuwa katika kutambua mchango wa wakandarasi ni mara
ya kwanza kwa mkutano huo kutokea Tanzania katika tasnia hiyo na mgeni
rasmi katika mkutano huo atakuwa katibu mkuu wa sekta ya ujenzi kutoka
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Injinia Joseph Nyamuhanga.
No comments:
Post a Comment