Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala,
Mheshimiwa George Mkuchika akisoma Taarifa ya Maboresho ya Mfumo wa
Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS) wakati Kamati hiyo ilipokutana
na Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mjini Dodoma. Kulia
kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Laurean Ndumbaro.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
akifuatilia majadiliano ya Wajumbe wa Kamati yake wakati Kamati hiyo
ilipokutana na Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala kwa ajili ya kupokea na kujadili Taarifa ya Maboresho ya
Mfumo wa Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS), Kulia kwake ni Katibu
wa Kamati hiyo, Eunike Shirima.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakiwa katika kikao
na Watendaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
ambapo leo walijadili Taarifa ya Maboresho ya Mfumo wa Utumishi na
Mshahara Serikalini (MCMIS), Kulia kwake ni Katibu wa Kamati hiyo,
Eunike Shirima.
No comments:
Post a Comment