Tuesday, October 10, 2017

Zawadi za shs milioni 204 kushindaniwa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC

 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala,  Sady Mwang’onda (wa pili kulia) na Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (wanne kushoto), wakikata utepe kuashirikia uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja hivyo kufanya jumla ya zawadi zote kufikia thamani ya shs milioni 204. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala,  Sady Mwang’onda (katikati), Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (kulia kwake), na Mkuu wa  Bidhaa na Wateja Rejareja, Andrew Lyimo (kushoto kwake), pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakishangilia mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC uliofanyika katika tawi hilo, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.
  Mkuu Bidhaa na Wateja Rejareja wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC uliofanyika katika tawi Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.
 Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda, Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji, Dorothea Mabonye, Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja, Andrew Lyimo
Wafanyakazi wa NBC Tawi la Mbagala pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo wakipozi kwa picha mbele ya gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ atakalojishindia mmoja wa washindi sita wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Washindi wengine 24 watajindishindia pesa taslimu shs milioni moja kila mmoja. 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...