Tuesday, November 03, 2015

WATALAAM WA TAKWIMU BARANI AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM.

mku1
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza jana na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tano ambao umekutanisha watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
mku2
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afrika Kusini Risenga Maluleke akizungumza jana na waandishi wa habari kuhusu madhumuni ya mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambapo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
mku3
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambao wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Kushoto kwake ni Mtakwimu kutoka Kamisheni ya Uchumi Afrika Bw. Andry Andriantseheno.
mku4
Baadhi ya wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka barani Afrika wakifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...