Tuesday, November 10, 2015

MAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA AKABIDHIWA OFISI RASMI NA DKT. BILAL, AKAKABRIBISHWA RASMI NA WAFANYAKAZI WA OFISI YAKE.

sa1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Novemba 9, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula. Picha na OMR
sa2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Nov  9, 2015. Picha na OMR
sa3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jan Nov9 2015  Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
sa5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, ….baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, jana 9,2015. Picha na OMR
sa6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, jana 9, 2015. Picha na OMR
sa7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, janav 9, 2015. Picha na OMR
sa8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Maua kama ishara ya makaribisho, kutoka kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, wakati alipowasili kwa mara ya kwanza kwenye Ofisi yake na kupokelewa na wafanyakazi wake janav 9, 2015. Picha na OMR
sa9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Sazi Salula,wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi jana. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Eng. Angelina Madete. Picha na OMR
sa10
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, wakati akiondoka baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
sa11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili. Picha na OMR
sa12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregerewakati akiwasili. Picha na OMR
sa13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowasili kwenye Ofisi hiyo baada ya makabidhiano. Akizungumza na wafanyakazi hao Mama Samia, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa bidii ili kutimiza Kaulimbiu ya Mhe.Rais ya ‘HAPA KAZI TU’. Picha na OMR
sa15
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza. Picha na OMR
sa17
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wanamama wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza kwa makabidhiano ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu. Picha na OMR
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekabidhiwa rasmi ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Baada ya makabidhiano hayo Mhe. Samia, alikaribishwa na watumishi wa ofisi yake ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii kulingana na kauli mbiu ya ‘Hapa ni Kazi tu’.
“Kila mmoja afanye kazi kwa bidii mahala pake pa kazi. Wale ambao kauli mbiu ya Hapa ni Kazi tu, itawapita wakae pembeni… watatusamehe”, alisema Makamu wa Rais
Aidha Mhe. Samia alisisitiza suala la kuendelea kupendana na kushirikiana miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ili kufanikisha azma ya kuleta matarajio ya maendeleo ya Watanzania wanayotaka kuyaona katika uongozi wa awamu ya tano.
Baada ya kutoa nasaha hizo alifanya kikao na Menenjimenti ya ofisi ambapo alitoa uelekeo wa utendaji kazi katika ofisi hiyo hususan kuzingatia kusimamia masuala ya muungano na mazingira ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Aliitaka Menejimenti hiyo kujipanga upya na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwa upande wa masuala ya muungano na mazingira.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
9/11/2015

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...