Rais Mh. Dk. John Pombe Magufuli akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaa leo kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni, Rais Dk. John Pombe Magufuli ameapa katika sherehe iliyohudhuriwa na marais mbalimbali wa Afrika wakiwemo Robert Mugabe wa Zamibabwe, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Joseph Kabila wa DRC Congo, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyata wa Kenya, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Edgar Lungu wa Zambia na wengine wengi wakiwemo mabalozi wa mataifa ya Ulaya, Marekani na taasisi za kimataifa ambao wameshuhudia sherehe hizo.
Dk.John Pombe Magufuli anakuwa rais wa awamu ya tano baada ya kupokea kijiti kwa watangulizi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na sasa Dk. Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyemuachia kijiti Dk. Magufuli.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Rais Dk. John Pombe Magufuli akipokea vitendea kazi kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande mara baada ya kuapishwa kwenye uwanja wa Uhuru leo, anayeshuhudia kushoto ni Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akipokea silaha za kijadi kutoka kwa mmoja wa wazee Mzee Job Lusinde mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akionyesha silaha za kijadi alizokabidhiwa mara baada ya kuapishwa kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa wamekaa mara baada ya kula kiapo kuitumikia nchi kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mstaafu Dk. Gharib Bilal na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa Rais kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akielekea kukaa mara baada kusalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, Rais wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe, Rais wa Uganda Mzee Yoweri Museveni na Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame.
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride kwa mara ya mwisho mara baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi wa Tanzania kwa miaka 10 na kumkabidhi kijiti Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Dk Jakaya Kikwete akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za kumuapisha Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Msafara wa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ulipokuwa ukiingia uwanjani tayari kwa shughuli za kumuapisha Rais Dk. John Pombe Magufuli .eo kwenye uwanja wa Uhuru.
Umati wa wananchi waliojitokeza katika sherehe hizo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akielekea eneo la kuapishwa.
Kadinali Policarp Pengo na Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk. Alex Malasusa wakielekea katika eneo la kuapishia.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande na Spika wa Bunge mama Anne Makinda wakielekea katika aneo la kuapishia.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema akiiongoza familia ya Rais Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete wakati familia hiyo ilipowasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais Paul Kagame wa Rwanda akielekea jukwaani mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru ili kushuhudia sherehe za kumuapisha Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Rais Mzee Robert Mugabe akielekea jukwaani mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Rais wa Afrika ya Kusini Mh. Jacob Zuma akisalimiana na Marais wastaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin Mkapa.
Rais wa Afrika ya Kusini Mh. Jacob Zuma akiwasalimia viongozi mbalimbali wakati alipowasili uwanjani hapo aliyekaa wa pili kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Janet Magufuli.
Viongozi mbalimbali serikali na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa katika sherehe hizo kwenye uwanja wa Uhuru.
Gwaride Maalum la vikosi vya JWTZ likipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na kutoa heshima mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na viongozi mbalimbali katika jukwaa kuu mara baada ya kuapishwa leo hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment