Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Ezra Ndangoya akimwelekeza sehemu ya kuweka sahihi Bw. Sironga Lowassa (kulia) ambaye ni mwombaji wa mkopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi.
Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Zahra Kitara (kushoto) akipokea viambatanisho vya maombi ya mkopo kutoka kwa Bw. Paul Yahhi (kulia) mwombaji wa mkopo ambaye fomu yake ya maombi ilikosekana baadhi ya viambatanisho jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi.
Maafisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) (kulia) wakiwahudumia waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi.
Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Christina Chacha (kulia) akimwelekeza jambo mwombaji wa mkopo ambaye fomu yake ya maombi ilikosekana baadhi ya viambatanisho jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi. (Picha na Eline Maronga-HESLB)
Na Eline Maronga
WAOMBAJI wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu zao za maombi zimegundulika kuwa na upungufu wameipongeza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuwapa fursa ya kufanya marekebisho.
Mwishoni mwa wiki iliyopita HESLB ilitangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi ziligundulika kuwa na upungufu na kuwataka waombaji kufika katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam na kufanya marekebisho kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).
Wakiongea katika ofisi za Bodi leo (Jumatano, Agosti 2, 2015), waombaji hao wamesema hatua hiyo ya Bodi imewawezesha kurekebisha fomu zao katika maeneo waliyokosea na hivyo kuweka kumbukumbu zao sawa.
“Mimi ninaishi Arusha na nilipata taarifa kupitia magazetini na nikatembelea tovuti ya Bodi na kuona jina langu kuwa sikuweka sahihi… nikaamua kuja na sasa nimeweka sahihi,” amesema Bw. Sironga Lowassa leo nje ya Ofisi za HESLB.
No comments:
Post a Comment