Monday, February 17, 2014

TUZO ZA KILI 2014 ZIMEZINDULIWA LEO

George Kavishe.
Ni time ya kufahamu kuhusu tuzo ambazo hutolewa kwa Wanamuziki/Wasanii mbalimbali wa Tanzania zikiwa zimeanzishwa mwaka 1999 ambapo za mwaka huu 2014 zimezinduliwa leo February 17.
George Kavishe kutoka TBL ambao ndio Wadhamini wa tuzo hizi amesema  ‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu ni tofauti na mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga kura tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category gani, mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani’
‘Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao kupitia simu ya mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye kipengele’ – Kavishe
‘Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura mara mbili ambapo ya kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena kupiga kura nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama wimbo uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’ – Kavishe
MABADILIKO: Kwa mujibu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA), mabadiliko yaliyofanywa kwenye tuzo za mwaka huu wa 2014 ni kutokana na maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki kutoa sababu mbalimbali.
Mwaka huu KTMA itakua na category 36 ambapo category 34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.
Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka huu imeondolewa moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo category yenyewe ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014 ni Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume mwaka jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya mwaka jana Msanii bora wa kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume  band ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume band, mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya mwaka jana msanii bora wa kike bongofleva.
Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka jana msanii bora wa kike Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.
BASATA wanasema ‘kwa nini kumekua na mabadiliko haya? ukiangalia maana halisi ya neno Msanii linasadifu au linaleta maana za kuingia zaidi ya kitu kimoja, kunaweza kuwepo na msanii wa uchongaji, msanii wa Uchoraji n.k kwa sababu wanafanya kazi ya sanaa ndio maana tunatumia majina ya kimuziki kwa sababu huku tuko kwenye muziki’
MENGINE
BASATA wanasema ‘mwaka huu tutakua na video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo, neno muziki lina uwanja mpana kuliko wimbo…….. pia tutakua na wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili’
‘Jingine ni Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia…. wapo wasanii wengi sana chipukizi huko mtaani na miziki yao haijasikika, inawezekana amekaa miaka mingi akifanya kazi zake lakini akaibuka na ameonekana’ – BASATA
CHANZO NI MILLARDAYO

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...