Thursday, February 06, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA OFISI YA IECO UKANDA WA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam  Tanzania, kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam  Tanzania,  kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...