Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mwanza Ziwa Victoria (DMZV) Andrew Gulle kabla ya kufunua jiwe maalum la Jubilee alikata utepe kuashiria safari ya maadhimisho hayo kuanza rasmi, ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 31 Agosti, 2014.
Maaskofu waalikwa toka makanisa mbalimbali kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Baada ya tukio la kuzindua jiwe la Jubilee Maaskofu na mamia ya waumini walielekea kwenye jengo la Kanisa kuu la Mwanza kwaajili ya kulizindua.
Kabla ya Uzinduzi wa kanisa la Imani KKKT Mwanza historia ya ujenzi wa kanisa hadi kukamilika ilisomwa naye Bw. Serafin Kimaro. Jumla ya shilingi bilioni moja na milioni 500 zimetumika kukamilisha ujenzi huo uliotumia miaka takribani 13 hadi kukamilika.
Akishuhudiwa na mamia ya waumini na viongozi wa makanisa mbalimbali Kanda ya ziwa na mikoa mingine nchini ukafika wakati sasa wa mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa kukata utepe kuzindua kanisa la KKKT Imani Makongoro Mwanza.
Kisha mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa aligonga malango ya kanisa na kuingia ndani kwa mara ya kwanza ikiwa ni rasmi.
Mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa alikuwa ni wa kwanza kuongoza msafara wa maaskofu, wachungaji na mamia ya waumini waliohudhuria Jubilee hiyo.
Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa (kulia) akiongoza ibada ya kuweka wakfu kanisa la KKKT Imani Makongoro akiwa ameambatana na Askofu Andrew P. Gulle wa Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV) katikati aliyemshikia kipaza sauti.
Ibada inaendelea.
Kwaya ya Imani KKKT.
Wageni toka mataifa mbalimbali ulimwenguni nao pia wameshiriki maadhimisho ya Jubilee hiyo.
Kwaya alikwa ya KKKT Kijitonyama toka jijini Dar es salaam iliipamba Jubilee.
Nyimbo nzuri nzuri zilisikika.
Wanamuziki wa KKKT Kijitonyama.
Maandari ya kanisa toka juu na upande wa kulia.
Kushoto na kulia hadi mbele kwenye madhabahu.
Kanisa hili limejengwa kwa nguvu za waumini wa ushirika wa Imani, waumini wa sharika nyinginezo na marafiki wa usharika huo na DMZV.
Sehemu waliyoketi Kamati ya maandalizi ya Jubilee na Ujenzi.
KKKT Imani wakitoa huduma ya kiroho kwa njia ya uimbaji.
Sherehe za Jubilee ya miaka 25 ya DMZV ziliambatana na harambee ya ujenzi wa Imani Lutheran Schools mradi endelevu unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili za kitanzania hadi utakapokamilika.
Harambee ilifanyika ikiwa na makusudi ya kukusanya zaidi ya shilingi milioni 250 kwaajili ya kuanza ujenzi ambapo kamati ilivuka malengo kwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 259,280,000/= zikiwemo ahadi, na taslimu ilikuwa kiasi cha shilingi milioni 58,869,000/=.
Harambee ilifanyika ikiwa na makusudi ya kukusanya zaidi ya shilingi milioni 250 kwaajili ya kuanza ujenzi ambapo kamati ilivuka malengo kwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 259,280,000/= zikiwemo ahadi, na taslimu ilikuwa kiasi cha shilingi milioni 58,869,000/=.
No comments:
Post a Comment