Thursday, February 27, 2014

Rais Jakaya Kikwete amteua Bwana Togolani I. Mavura kuwa msaidizi wa Rais (Hotuba)

 Togolani Mavura
--

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Togolani I.Mavura kuwa msaidizi wa Rais (Hotuba) kuanzia Februari 8,mwaka huu, 2014. 

Taarifa iliyotolewa Jumanne, Februari 25, 2014,mjini Dar es Salaam na katibu mkuu kiongozi,Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Bwana Mavura anachukua nafasi ya Bwana Msafiri Marwa ambaye amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa na kupangiwa kazi nyingine.

 
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mavura ambaye ni ofisa wa mambo ya nje alikuwa Katibu wa Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 


Imetolewa na,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar Es Salaam

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...