Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya Stendi-kata ya Ifunda.
Mapokezi Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.
Mh:Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda.
Chief Wa Wahehe, Chief Mkwawa ambaye pia ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akishikana Mikono ya Baraka na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Godfrey William Mgimwa,Pia akisalimana na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya Ifunda-Kalenga.Kubwa zaidi CHIEF MKWAWA ambaye ni Mtoto wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.
Msanii Dokii ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi akitumbuiza kwenye ufunguzi wa kampeni wa Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi.Dokii ametunga wimbo rasmi kwaajili ya Kalenga na Umuhimu wa Kijana Godfrey William Mgimwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,
Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Ndugu Mtatulu akionesha baadhi ya Mitego inayodaiwa kuwekwa na Vijana wa CHADEMA kwenye njia ili Magari ya CCM yanayozunguka kwenye Kampeni yapata matatizo.Pia Ndugu Mtatulu alitaja majina ya Wahusika na ameshayapeleka Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Kijana Godfrey William Mgimwa ambaye ni Mgombe Ubunge Jimbo la Kalenga.
Wabunge wa Iringa(Wilaya+majimbo) wakitoa neno la kuomba Kura kwa Wananchi Wa Ifunda ili wamchague Mgombe wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa.
Ni Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na mamia ya Wananchi waliofurika Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda hii leo kuhudhuria Mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga(CCM).Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wananchi wa Kalenga kumchagua Kijana Godfrey William Mgimwa kwa sababu anakila sifa za kuwatumikia Wananchi wa Kelenga,Lakini pia ni Kijana aliyependekezwa na Chama kuanzia ngazi ya Chini hadi Taifa kwa mtindo wa Kura za maoni na amewashinda wenzake 9.
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo.
Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza.
Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.
Kijana huyu ameamua kurudisha Kadi ya Chadema baada ya Somo zuri Kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la Kalenga.
Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa hii leo kwenye Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la kalenga.Uchaguzi unategemewa Kufanyika tar.16/03/2014.
Picha zote na Habari kwanza Blog
No comments:
Post a Comment