Friday, February 21, 2014

Picha Mbalimbali Kutoka Bunge Maalum La Katiba Mjini Dodoma

Waziri wa Sheria na Katiba ambaye pia ni mjumbe wa Bunge  maalum la Katiba Dkt Asharose Migiro (kushoto) na Mjumbe wa Bunge  maalum la Katiba Hamad Rashid wakibadilishana mawazo jana mjini Dodoma wakati wakielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe (kulia) na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Thomas Kashilila (kushoto)  wakibadilishana mawazo jana mjini Dodoma wakati wanaelekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo  ambaye pia  ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Juma Mkamia  na Mjumbe Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Joshua Nasari wakibadilishana mawazo jana mjini Dodoma mara baada ya uwasilishaji wa rasimu  ya kanuni za Bunge Maalum    Katiba.
 Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Profesa Ibrahim Lipumba(kushoto) na Mwenyekiti wa CHAUSTA na ambaye ni Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba James Mapalala(kushoto) wakibadilishana mawazo jana mjini Dodoma mara baada ya uwasilishaji wa rasimu  ya kanuni za Bunge Maalum   Katiba.
 Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo  ambaye pia  ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba  Dkt Fenelaa Mkungala (kushoto) na Mwanasheia Mkuu wa Serikali Jaji  Fredrick Werema (wa pili kushoto) na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Yusuph Singo (kulia) na Dkt. Franicis Michael (wa pili kulia) wakibadilishana mawazo jana mjini Dodoma mara baada ya uwasilishaji wa rasimu  ya kanuni za Bunge Maalum    Katiba.
 Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Profesa Ibrahim Lipumba(mwenye suti ya kijivu) akibadlishana mawazo na waandishi wa habari jana mjini Dodoma kabla ya kuingia katika ukumbi wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba.
 Baadhi  ya wajumbe wa Mkutano wa Bunge  maalum la Katiba wakiwasili katika Ukumbi wa Bunge jana mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano.
  Baadhi  ya wajumbe wa Mkutano wa Bunge  maalum la Katiba wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa rasimu  ya kanuni za Bunge Maalum  jana mjini Dodoma .
 Waziri Mkuu na ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Mizengo Peter Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Balozi Seif  Alli Iddi wakifuatia uwasilishaji wa rasimu ya rasimu  ya kanuni za Bunge Maalum    jana mjini Dodoma
Waziri Mkuu na ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Mizengo Peter Pinda akibadilishana mawazo jana mjini Dodoma  na wajumbe wenzake mara baada ya kuharishwa kwa kikao.Picha na Idara ya Maelezo-Dodoma

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...