Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Badra Masoud akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kwamba shirika hilo kuwa hatarini kupelekwa mahakamani kufuatia kuvunja mkataba na kampuni ya McDonald Live Line Technology Limited iliyoshindwa kutekeleza zabuni iliyopewa kwa mujibu wa mkataba kati ya Pande hizo,kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo bw. Frank Mvungi.
----
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Limekanusha taarifa iliyotolewa na baadhi ya habari kuwa liko mbioni kufikishwa mahakama kutokana na kuvunja mkataba na kampuni ya McDonald Live Line Technology Limited.
Akikanusha taarifa hiyo Meneja Uhusiano wa shirika hilo Badra Masoud amesema kuwa shirika liliamua kuvunja mkataba na kampuni hiyo baada ya kushindwa kutekeleza zabuni waliyopewa ya kusafirisha, kusambaza na kuweka nguzo za umeme katika eneo la Kiyungi/Arusha 06 kV lines iliyotakiwa kukamilika ndani ya wiki 32 kuanzia Julai 28, 2010 na kuisha mwezi Machi 11, 2011.
Badra aliongeza kuwa baada ya mkataba huo kuvunjwa kampuni ya McDonald ilifungua shauri katika Tume ya Usuluhishi na Ushindani ambapo mara baada ya pande zote kusikilizwa kampuni hiyo iliamriwa kuilipa TANESCO fidia ya zaidi ya milioni 700.
No comments:
Post a Comment