Thursday, December 05, 2013

:Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga awasilisha Hati za Utambulisho nchini Comoro

 Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro akisoma Hati za Utambulisho za Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga, katika Ikulu ya Beit Salaam, Moroni.
Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine wa Muungano wa Visiwa vya Comoro akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi huyo. 
----


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga,juzi tarehe Desemba 2013 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Beit Salaam, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Rais Dhoinine walipata fursa ya kuzungumza machache katika muktadha wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya Tanzania na Comoro kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...