Wednesday, December 11, 2013

Mwanasheria wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando kuzungumza leo na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi)

   
MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo
 MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Albert Msando
Samson Mwigamba
-----
MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi).


Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu  ya mashitaka 11 na majibu yake  ambayo Mhe. Zitto Kabwe  na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama. 


Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.


Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,

Jumanne, 10 Desemba 2013

Dar es Salaam

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...