Jeneza lenye mwili wa Mandela likielekea kwenye eno la mazishi katika kijiji cha Qunu mapema leo
Sura za huzuni za Graca Machel (juu) na Winnie (chini) wakiwa mazishini
Nelson Mandela 1918 - 2013
Mazishi ya mzee Nelson Mandela ymekwishafanyika katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa huyu wa Afrika mzee Nelson Mandela.
Idadi ya Takribani watu 4,500 wakiwemo wageni wa kimataifa wamehudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale huku wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa.
Moja kati ya mataifa yaliyopata heshima ya kuongea mbele ya viongozi mbalimbali duniani ni Rais wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Eneo analozikwa mzee Nelson Mandela ni sehemu ya makaburi yaliyo kwenye shamba kubwa la familia ya Mandela lililoko katika kijiji cha Qunu lililojengwa mara baada ya kuachiliwa kutoka jela mwaka 1990, katika eneo lenye nyasi za kijani , na milima ya Cape ya mashariki.
No comments:
Post a Comment