Makamu Mkuu wa Chuo KIkuu cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Ricky Mahalu
----
MAKAMU Mkuu wa Chuo KIkuu cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Ricky Mahalu anawatangazia mahafali ya kwanza ya kihistoria ya chuo hicho, yatakayofanyika Jumamosi Desemba 7 mwaka huu, Saa nne asubuhi katika Makumbusho ya Taifa karibu na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Dar es Salaam.
Profesa Mahalu aliyasema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Chuo hicho, Mikocheni B kwa Warioba, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohammed Gharib Bilal.
Profesa Mahalu alisema chuo hicho kilianzishwa rasmi miaka miwili na miezi mitatu iliyopita ambapo hadi sasa ina jumla ya wanafunzi zaidi ya 850. Kwani wakati kilipoanzishwa mwaka 2011 chuo kilianza na wanafunzi wa 65.Hadi sasa wana jumla ya koleji nne , koleji ya kwanza ni ya Sheria, Ualimu, Sayansi Uchumi na sayansi ya Menejimenti.
Hata hivyo alitoa wito kwa waandishi wa habari wote nchini waone wakati umefika sasa wakuanza kupenda kusoma fani ya sheria kwani wasomi wa sheria na jamii imekuwa ikishuhudia baadhi ya habari zinazohusu masuala ya kisheria kama habari za mahakamani zikilizipotiwa hisivyosahihi na baadhi ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa endapo waandishi wengi wa habari waamue kusoma sheria wangeondokana na tatizo hilo la kutokufahamu vyema kuripoti habari zinazohusu masuala ya kisheria.
Aidha alisema tayari waandishi wa habari za mahakamani wawili nchini wameishajiunga katika chuo hicho na wanasoma kozi ya shahada ya sheria na kwamba chuo kinashuhudia mabadiliko makubwa sana ya uandishi wenye radha ya kisheria unaonandikwa na waandishi hao katika vyombo vyao vya habari kwasababu wanasoma sheria.
No comments:
Post a Comment