Friday, December 20, 2013

MAMA SALMA APOKEWA KWA SHANGWE BAADA YA KURUDI NA TUZO YA UONGOZI KUTOKA DUBAI

IMG_1756Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja kumpokea tarehe 19.12.2013IMG_1779 (1)Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi IMG_1790Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ofisi za WAMA, ambako mamia ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya kumpongeza baada ya kurudi na Tuzo ya uongozi aliyopokea huko Dubai tarehe 18.12.2013.IMG_1795Baadhi ya wananchi walioshiriki mapokezi ya Mama Salma wanaonekana wakimsikiliza wakati alipokuwa akiwahutubia katika viwanja vya WAMA tarehe 19.12.2013.IMG_1834Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi waliofika kumpokea aliporejea kutoka Dubai tarehe 19.12.2013.  Mama Salma alienda huko kupokea Tuzo ya uongozi ulitukuka kutokana na kazi anazofanya kupitia Taasisi yake kwa ajili ya elimu kwa wanaotoka katika mazingira magumu, afya ya mama na mtoto pamoja na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.IMG_2046Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiongea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Raymond Mushi wakati wa shamrashamra za kumpokea Mama Salma baada bya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kupokea TUZO ya uongozi uliotukuka. Tuzo hiyo hutolewa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi, (CELD).
IMG_2026Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza na wananchi waliofika kumpokea kwenye ofisi za WAMA tarehe 19.12.2013.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

No comments: