Sunday, December 08, 2013

MHE. ANGELA KAIRUKI ATAJWA KUWA MIONGONI MWA WANAWAKE VIJANA 20 WENYE NGUVU BARANI AFRIKA 2013

Mhe. Kairuki
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Angela Jasmine Kairuki (37) ametajwa katika  jarida la kimataifa la Forbes kuwa ni mmoja wanawake vijana 20 wenye nguvu barani Afrika mwaka huu. 
 
 Katika toleo lake la hivi karibuni chini ya kichwa cha habari ‘The 20 Young Power Women in Africa 2013’, jarida la Forbes linamuorodhesha Mhe Kairuki sambamba na wanawake wengine 19 kama vijana wa kike wenye nguvu kwa nafasi zao kikazi na kibiashara. 
 
Kutajwa kwa Mhe Kairuki katika orodha hiyo kumezua msisimko katika mawasiliano ya mtandao wa ‘twitter’ ambapo Watanzania wengi wamekuwa wakielezea furaha na fahari zao kwa kuona Mtanzania mwenzao, tena mwanamke kijana, anatambulika kimataifa kwa utendaji wake.
 
Mhe. Angela Kairuki akitembelea Jeshi la Magereza
katika mojawapo ya shughuli zake za kikazi
 Wanawake wengine waliotajwa na jarida hilo ni Mimi Alemayehou (Ethiopia) Makamu wa RAis Mtendaji wa Overseas Private Investment Corporation (OPIC),   Vera Songwe(Cameroon) Mkurugenzi Mkazi World Bank Senegal, na Tara Fela-Durotoye (Nigeria) Mwanzilishi wa House Of Tara.
Wengine ni  Rapelang Rabana (Afrika Kusini) Mjasiriamali,   Claire Akamanzi (Rwanda) Afisa Mtendaji Mkuu wa Rwanda Development Board,   Valentina da Luz Guebuza (Msumbiji) Mwekezaji,  Hadeel Ibrahim (Sudan) wa Mo Ibrahim Foundation,  Alengot Oromait (Uganda) Mbunge, na   Monica Musonda, (Zambia) Afisa Mtendaji Mkuu na MWanzilishi wa kampuni ya Java Foods. 
Wengine ni NoViolet Bulawayo (Zimbabwe) Mtunzi wa vitabu, Minoush Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, mjasiriamali na mwendesha benki,  Ola Orekunrin (Nigeria) Daktari na Mwanzilishi wa The Flying Doctors,  Sibongile Sambo (Afrika Kusini) Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa SRS Aviation,  Lupita Nyong’o (Kenya) Mwigizaji na mtengeneza filamu,    Amini Kajunju (Congo DRC) Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Africa-America Institute na  Folake Folarin-Coker (Nigeria) Mbunifu wa mitindo.
 
Wengine katika orodha hiyoni  Lindiwe Mazibuko (Afrika Kusini) Mwanasia na Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA) bungeni,   Minoush Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, Mjasiriamali na mwendesha benki,  Sibongile Sambo (Afrika Kusini),  Wangechi Mutu, (Kenya) Msanii na mchongaji.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...