Thursday, December 12, 2013

JENERALI MSTAAFU WAITARA APOKEA WAPANDA MLIMA WA ‘UHURU EXPEDITION’ NA KUWATUNUKU VYETI

Photo 1 chtMkuu wa JWTZ msataafu Jenerali George Waitara (kulia) akimtunuku Mwenyekiti wa TTB Balozi Charles Sanga cheti baada ya kushiriki kupanda mlima Kilimanjarao katika kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Anayeshuduia kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa KINAPA Bwana Erastus Lufungulo
Photo 2 chtJenerali Waitara (kulia) akimtunuku cheti Meja Jenerali Christopher Gimongi ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa wapanda mlima wa ‘Uhuru Expedition’ mua mfupi baada ya wapanda mlima hao kukamilisha zoezi hilo hapo jana.
Photo3Wapanda mlima kutoka TTB, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Jenerali mstaafu George Waitara (mwenye jaketi jeupe), waongoza wapanda mlima, na Mkuu wa Hifadhi ya KINAPA muda mfupi baada ya kukabidhiwa vyeti.
…………………………………………………………………………………………
Na Geofrey Tengeneza
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi  Tanzania-JWTZ  Jenerali mstaafu George Waitara ameihakikishia Bodi ya Utalii Tanzania –TTB kuwa Jeshi hilo litaendelea kuunga juhudi za TTB katika kuvitangaza vivuto vya Utalii vya Tanzania ukiwemo mlima Kilimanjaro kupitia msafara wa kupanda mlima Kilimanjaro maarufu kwa jina la Uhuru Expedition unaofanywa na Jeshi la Wananchi kila mwaka katika kuadhimisha Uhuru wa Tanzania.
Jenerali Waitara ambaye ndiye Kiongozi na msimamizi mkuu wa  Uhuru Expedtion aliyasema hayo jana wakati akiwapokea wapanda mlima walioshiriki katika msafara huo mwaka huu ulioratibiwa na kufadhiliwa na Bodi ya Utalii Tanzania katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro –KINAPA Marangu Moshi. “Tunaishukuru sana Bodi ya Utalii kwa kushirikiana nasi kwa mara nyingine tene katika msafra huu, lakini pia nawashukuru sana KINAPA kwa msaada wote waliotupa na niwahakikishie kuwa Jeshi litaendelea kuutangaza utalii wetu wa Tanzania ukiwemo utalii wa kupanda mlima Kilimnjaro” alisema Jenerali msataafu Waitara ambaye pia  aliwakabidhi vyeti wapanda mlima sita.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Balozi Charles Sanga ambaye pia alikuwa miongoni mwa wapanda mlima alisema kuwa Bodi ya Utalii inafurahi kuona kuwa Uhuru Expeditioniliyoasisiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania inaendelea kuimarika na kutekeleza malengo ya kuanzishwa kwake na kwamba kwa kutambua mchango wa Expedition hii ndiyo maana TTB imekuwa ikiiunga mkono. Amemsifia Jenerali Waitara kwa kuisimamia vema Expediton hii na kwa juhudi zake za kuhakikisha kila mwaka tukio la kupanda mlima la Uhuru Expedition linafanyika.
Naye Kiongozi wa Msafara uliopanda mlima mwaka huu Meja Jenerali Christopher Gimongi amesema msafara huu uliokuwa na wapanda mlima saba ulianza kupanda mlima tarehe 6/12/2013 kupitia njia ya Marangu na kwamba ni wapanda mlima watatu tu akiwemo yeye walioweza kufika kileleni. Meja Jenerali Gimongi alisisitiza umuhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufadhili Uhuru Expedition kama alivyoahidi Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki wakati wa tukio kama hilo kama mwaka jana.
Tukio la kupanda mlima mwaka huu kupitia Uhuru Expedition lilishirikisha wafanyakazi wawili wa TTB, Mwenyekiti wa TTB baolzi Charles Sanga, Meja Jenerali Mstaafu Christopher Giomongi na wafanyakazi watatu kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwemo mwanamke mmoja.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...