Friday, November 15, 2013

WANANCHI KUSINI WATAKA KOROSHO IBANGULIWE NCHINI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Viongozi wa CCM pamoja na wananchi wa wilaya ya Tunduru mara baada ya kuwasili kwenye wilaya hiyoikiwa sehemu ya ziara yake ndefu katika mikoa ya kusini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia mikono na wananchi wa kijiji cha Nakapanya,wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Wananchi wakazi wa kijiji cha Nakapanya wakionyesha Korosho kama sehemu ya kilio cha cha muda mrefu ambacho kimekuwa hakisikilizwi ipasavyo,wananchi hao walimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa uamuzi wake wa kulisemea na kuahidi kulishughulikia kwa Chama kuibana Serikali juu ya masuala muhimu ya zao la krosho kwa kutasaidia sana kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama wa Chama cha CUF ambao wameamua kurudi rasmi CCM wakiongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Sheikh Ally Hashim.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Nakapanya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi ilishatoa tamko la kuitaka serikali ishughulikie matatizo ya zao la korosho mara moja na kusisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi hivyo ni jukumu la chama kuwatetea wakulima wa Korosho walipwe kwa wakati na kwa bei nzuri,pia Korosho zibanguliwe nchini kwani zitaongeza thamani yake na pia kupanua wigo wa ajira.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Nakapanya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi za kata ya CCM Namiungo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa Namiungo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM ya Kata,wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Tarehe 14 Novemba 2013. Picha na Adam H.Mzee

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...