Tuesday, November 19, 2013

AUA WAWILI KWA KUWAPIGA RISASI KISHA AJIUA


Mtu anayedaiwa kuwa ni Mfanyabiashara wa jijini Mwanza, na kufahamika kwa jina la Gabriel Munisi amejiua baada ya kushambulia watu wanne kwa risasi asubuhi ya leo eneo la Ilala Bungoni jirani na Klabu ya Wazee.

Shambulizi hilo linaelezwa kuwa ni la kimapenzi limefanywa na Munisi baada ya kubaini nyendo za ndivyo sivyo kwa mpenzi wake aliyetajwa kwa jina la Christina Nando.

Imeelezwa kuwa Mtu huyo aliwashambulia kwa risasi wakiwa ndani ya gari wakitoka ndani hivyo kumpiga risasi dereva wa gari hilo, Francis Samwel, Christina Nando na watu wengine wawili waliokuwapo ndani ya gari hilo ambapo mmoja ni mama mzazi wa Christina.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema watu watatu walifariki kutokana na tukio hilo. 
Jamaa Aliyehusika na Mauwaji
TAARIFA ZAIDI 
Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.

Dereva mmoja wa taxi kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.
 

Kwa mujibu wake dereva huyo aliendelea kusimulia, alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM. 


Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba, aliendelea kusimulia dereva huyo.
 

Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari mama mmoja na wadada wawili.
 

Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol, hii ni kwa mujibu wa dereva huyo na mara baada ya kuona hivyo hivyo ikabidi akimbie.
 

Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia limpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.
 

Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
 

Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauwaji hayo licha ya watu wengi ambao nilipata bahati ya kuongea nao wakilihusisha tukio hilo na mambo ya kimapenzi. SOURCE: DANCHIBO BLOG.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...