Kibanda akielekea kupokea tuzo huku akila kwa uchungu |
Kibanda akibembelezwa na mmoja kati ya majaji wa tuzo hioy |
Na Francis Godwin Blog Mwanza
Mshindi wa tuzo yakishujaa na uandishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi Absalom Kibanda leo amewaliza wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) baada ya kushindwa kusimama kupokea tuzo hiyo yenye thamani ya Tsh milioni 10 na badala yake kuangua kilio kwa uchungu ukumbini hapo.
Tukio hilo ambalo ni la kwanza katika histori ya washindi wa tuzo mbali mbali kutokea nchini limetokea leo katika Hotel la JB jijini Mwanza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hiyo iliyotolewa na UTPC.
Kibanda ambae muda wote alionekana kutulia katika nafasi yake hadi pale jiji mkuu wa tuzo hiyo mwanahabari maarufu nchini Tanzania Hamza kasongo kupita mbele na kusoma sifa za mshindi wa tuzo hiyo na kumwita mmoja kati ya majaji kutaja jina la mshindi .
Baada ya kibanda kutangazwa mshindi hakuweza kuonyesha furaha kama ilivyo kwa washindi wengine na badala yake kuanza kulia kwa uchungu kiasi cha baadhi ya wajumbe ukumbini hapo akiwemo makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanjo kuungana nae kuangusha chozi ukumbini hapo na kufuatiwa na wajumbe mbalia mbali akiwemo mjane wa Mwangosi Bi Itika Mwangosi .
Baada ya kibanda kutangazwa mshindi hakuweza kuonyesha furaha kama ilivyo kwa washindi wengine na badala yake kuanza kulia kwa uchungu kiasi cha baadhi ya wajumbe ukumbini hapo akiwemo makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanjo kuungana nae kuangusha chozi ukumbini hapo na kufuatiwa na wajumbe mbalia mbali akiwemo mjane wa Mwangosi Bi Itika Mwangosi .
Kutokana na hali hiyo zoezi hilo lilisogezwa mbele na kupigwa wimbo maarum wa kumkumbuka Mwangosi na baada ya hapo Kibanda alikaribishwa kukabidhiwa tuzo yake.
Hata hivyo Kibanda alionyesha kuwa na simanzi nzito na hata kuueleza umma uliokuwepo hapo kuwa tuzo hiyo inamtia majonzi zaidi kwa kukumbuka kifo cha Mwangosi na yale yaliyomkuta yeye kwa kuvamiwa na kutoborewa jicho lake .
Hivyo alisema mbali ya kesio hiyo kuendelea kuzunguswa bado yote anamwachia Mungu aliyemfanya kuwa hai hadi leo na kuwa katika fedha alizopata za tuzo asilimia 10 atamrejeshia mwenyezi Mungu na fedha inayobaki atagawana nusu kwa nusu na mjane wa Mwangosi
wakati huo huo wanahabari nchini wametakiwa kujenga umoja katika kupinga sheria kandamizi ya vyombo vya habari na wanahabari nchini inayatarajia kupitishwa na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Meneja wa uthibiti wa ubora kutoka baraza la habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya kishujaa na uandishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi .
Mtambalike amesema kuwa idadi ya waandishi kutekwa na kuuwawa imezidi kuongezeka hapa nchini huku kasi ya serikali kuvifungia vyombo vya habari pia inaendelea kuongezeka .
Hivyo iwapo wanahabari nchini hawataungana katika kupinga manyanyaso dhidi ya vyombo vya habari na kupinga sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari na wanahabari suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini litaendelea kubaki ndoto.
No comments:
Post a Comment