DMK, Alex Kassuwi na Davis Mosha wakisubiri mwili wa Martha Airport October 30, 2013
---
SHUKRANI
Na Alex Kassuwi
Ndugu zangu hadi hivi sasa siamini yaliyotokea, bado haijaingia akilini kama mke wangu mpenzi Martha Shani hatunaye tena! Siamini kama Martha amefariki! Naona yupo. Ndugu zangu kwa sasa nipo katika kipindi kigumu sana, nikiwa mwenyewe nikiangalia watoto machozi yanitoka. Maneno ya kinywa changu hayawezi kuelezea kuugua kwa nafsi na roho yangu.
Ndugu zangu, |Mama zangu, kaka zangu, dada zangu, mashemeji zangu, wakwe zangu, marafiki na jamaa zangu pamoja na yote haya sina budi kutoa shukrani zangu kwa yote mliyonitendea kuanzia maombi hospitali, kuwa nasi kipindi chote cha msiba mpaka kuusafirisha na kuuhifadhi mwili wa mpenzi wangu nyumbani Tanzania ambapo tulizika Alhamis Oktoba 31,2013 huko Puma Singida.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Natoa shukrani za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kuwezesha makaratasi ya kuusafirisha mwili wa mpenzi mke wangu.
Shukrani kwa wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kutununulia tiketi tatu za ndege, mimi na watoto wangu wawili.
SHUKRANI KWA VYOMBO VYA HABARI
Navishukuru sana vyombo vyote vya habari vilivyoshiriki kuhabarisha juu ya msiba huu. Vyombo ni vingi sana siwezi taja majina ya vyombo vyote nafasi haitoshi, nawashukuru sana wanahabari wote. Bali sina budi kutoa shukrani za pekee kwa Swahilitv blog, DJ Luke wa Vijimambo blog, Mubelwa Bandio wa Changamoto yetu blog, Abou Shatry wa Swahilivilla blog, Sundayshomari blog, Lucy Patrick blog, DMk411 blog na Issamichuzi blog kwa kuweza kuwahabarisha watanzania wote.
SHUKRANI KWA WACHUNGAJI
Mch. Peter Igogo – Cathedral of Praise Church, Bowie, MD
Mch. Ferdinand Shideko – The Way of the Cross Gospel -|College Park, MD
Mch. Mathayo Malekela – Asssemblies of God –Georgia Ave, Silverspring, MD
Bishop Melchizedeck Maturlo – Bethel Kingdom Church- Hyattsville, MD
Mch. Solomon Ng’imba kutoka –Double Oak Community Birmigham Alabama
Mch. Nicodemus Hanje – Kutoka Birmigham Alabama
Mchungaji Jerry Price – International Community Church
SHUKRANI ZA PEKEE KWA KAMATI YA MAZISHI MAREKANI
Natoa shukrani za pekee kwa kamati nzima ya Mazishi Marekani ikiongozwa na Mwenyekiti Bw. Augustino Malinda.
SHUKRANI ZA PEKEE WATU BINAFSI MAREKANI
Natoa shukrani za pekee kwa Bw. Neto na Mkewe Bi. Kate kwa kuwa nami nyumbani walifika mara moja alipoanguka mke wangu, tumekaa wote hospitali masaa nane pamoja hadi mwisho, wengine waliofika hospitali ni Bw. MK (Dickson Mkama), Mrs. Mohamed, Bora, Bw. Julius Manase na Mkewe, Mchungaji Mathayo Malekela, Mchungaji Peter Igogo, Mch. Jerry Price, , Augustino Malinda, Jack, Mariamu na Mvuniwa, Dada Faith Isingo, Pamela Gea, Kwizera, Sekela, Jack Odong na wengine wengi siwakumbuki majina.
Shukrani pekee kwa Cedra Eaton na Mumewe Bw. Honesty Mulamula
SHUKRANI KWA WANAMAOMBI
Ndani na nje ya Marekani: Dada Nancy Mosha, Alex Dago Motion, Ruth Shani, Neto Mwimbwa, Kate, Mrs. Mohamed, Bora, Julius Manase na Mkewe, Mchungaji Mathayo Malekela, Mchungaji Peter Igogo, Mch. Jerry Price, Augustino Malinda, Mary Mgawe,Jack, Mariamu na Mvuniwa, Dada Faith Isingo, Kwizera, Sekela, Jack Odong, Theresia Kassuwi, Martha kilimba, Neema Shani, Joseph Shani, Noel Shani na Wana maombi wote.
SHUKRANI ZA PEKEE KWA KAMATI YA MAZISHI TANZANIA
Natoa shukrani zangu za dhati kwa kamati ya Mazishi ya Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Bw. Hamis Mpinda.
Alex Kassuwi, Davis Mosha, Muddy na Masanja Mkandamizaji
Natoa shukrani maalum kwa Davis Mosha na Mkewe (Dada Nancy) kuwa nasi bega kwa bega kuchangia kwa kiasi kikubwa kuusafirisha mwili wa mpenzi mke wangu toka Marekani hadi nyumbani Tanzania, Muhimu zaidi familia ya Davis Mosha wamekuwa faraja kubwa sana kwangu na kwa watoto wangu kwa msaada, upendo walionao na malezi kwa watoto wangu. Asante sana Davis Mosha na Dada Nancy.
Shukrani za Pekee Kwa Watu Binafsi Tanzania
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani walikuja msibani. Kutoka kushoto; Bw. Tairo,Mushi, na MarkD
Dada Olivia, Alex na Dada Georgia. Walipokuja nipa pole na kuwakilisha rambirambi za wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani Tanzania .
Dada Olivia, Alex na Dada Georgia
NATOA SHUKRANI MAALUM KWA
Bw. Hamis Mpinda na marafiki zake Bw. Dan Fundisha Ezekiel
Bw. John Langas
Bw. Vincent Mughwai
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani Tanzania
Wafanyakazi wa NHC Makao Makuu
Bwana na Bi. Ridhiwani Kikwete kwa msaada wao na upendo kwa watoto
Diwani wa CCM kata ya Pangani Kibaha Bi. Mwanaidi Maliki Kiongoli
Diwani wa CCM Puma Mhe. Ramadhani Kulungu
Diwani Ikungi CCM viti Maalum Mama Asha Mnjori
Kanisa la Pentekoste Puma
Mchungaji Peter Ihema wa kanisa la Kanisa la Pentekoste Puma,
SHUKRANI ZA PEKEE KWA TAASISI TANZANIA
1. NSSF
NAWASHUKURU SANA SHIRIKA LA NSSF KWA KUWEZA KUCHANGIA KUSAFIRGUGISHA MWILI WA MPENZI MKE WANGU MARTHA SHANI.
Bi. Eunice Chiume na
Bw. Crescentius Magori
2. IDEA ( Ikungu Development Association)
Nawashukuru sana wanachama wa IDEA kwa upendo na msaada wao.
3. SHAMBOGO FOUNDATIONShukrani za pekee kwa shambogo Foundation kwa kushiriki kikamilifu katika msiba wa mpenzi mke wangu.
MWISHO NATOA SHUKRANI KWA WATANZANIA WOTE WA NJE NA NDANI YA NCHI KWA MOYO WA UPENDO NA USHIRIKIANO
No comments:
Post a Comment