Monday, November 25, 2013

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Akutana Kwa Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya China Mh.Hong Yi IKULU Jijini Dar Es Salaam

 Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya Jamhuri ya Watu wa China Mh.Hong Yi akimkabidhi nakala ya kitabu chenye nasaha za watu mashuhuri kutoka jamhuri ya watu wa China  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Tanzania Profesa Joseph Semboja. Awali viongozi hao wawili walifanya mazungumzo yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Taasisi ya Uongozi ya China na ile ya Tanzania.Taassisi hizo mbili zinatarajia kutia saini mkataba wa ushirikiano wiki hii.
Katibu Mkuu balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya China Mh.Hong Yi ikulu jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Freddy Maro-IKULU
---
 
Taasisi ya Uongozi Tanzania(Uongozi Institute pamoja na Taasisi ya Uongozi ya China(Chinese Academy of Governance) zinatarajiwa kusaini Mkataba  wakukuza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili Jumanne wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Institute Profesa Joseph Semboja ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana baada ya Ujumbe kutoka Taasisi ya Uongozi wa China( Chinese Academy of governance) kumtembelea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo kutoka Jamhuri  ya Watu wa China unaongozwa na makamu wa Rais wa Taasisi hiyo Bwana Hong Yi na ziara hiyo inafuatilia ziara ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo pamoja na mambo mengine uhusino kati ya taasisi hizo mbili ulitiliwa mkazo.

Profesa Semboja aliongeza kusema kuwa mkataba wa mahusiano kati ya taasis hizo utawezesha ubadilishanaji wa teknolojia na utaalamu na hivyo kuboresha mafunzo yanayotolew na taasisi ya Uongozi Tanzania.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alimshukuru Bwana Hong Yi kwa nia yake njema ya kushirikiana na Taasisi ya Uongozi Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya China na Tanzania ni wakihistoria na wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo mbili.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...