Tuesday, November 12, 2013

Dk Bilal, azindua rasmi benki ya Maendeleo PLC jijini Dar leo


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic na Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mchungaji, George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa  kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Afisa Utawala wa Benki ya Maendeleo, Rose Mushi, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa  kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Wa pili (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene (kulia) ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa kadi ya ATM, mteja wa kwanza kufungua Account katika benki hiyo, Elianasa Marco Njiu,mkazi wa jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Nov 12, 2013. Wa pili (kulia) ni Mteja wa kwanza kupata mkopo katika benki hiyo, Margareth Chiwata.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa bemki hiyo,leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wachungaji wa Kanisa la KKKT, baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...