Friday, November 15, 2013

Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 yanaswa bandarini Zanzibar

 Baadhi ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na uzito kwa ujumla.
 Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo
 Askari wa jeshi la Polisi wakitoa Pembe za Tembo katika magunia wakati wa zoezi hilo jana asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
 Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.
 Operesheni Ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata thamani yake halithi.
 Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyo jana yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Magunia haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya Zanzibar jana asubuhi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...