Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(kulia) akibadilishana hati za makubaliano ya mikataba ya ushirikiano na Mwanzilishi wa kikundi cha kimataifa cha Vijana kutoka Korea(IYF) Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Mchungaji Mwandamizi huyo ambae ametia saini kwa niaba ya kikundi cha IYF(International Youth Fellowship) . Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara(katikati).
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo.Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Mwanzilishi wa IYF ya Korea Ock Soo Park , ambae pia ni Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa laGood News Gangnam.Dhumuni ya tuzo hiyo ni kwaajili yakumpongeza Mh,Waziri huyo kwa jitihada za kazi zake .
Picha ya Pamoja.
Picha ya Pamoja.
Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo imetiliana saini Mikataba ya Ushirikiano na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana cha ‘International Youth Fellowship (IYF)’ cha Korea.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Sihaba Nkinga ametia saini Mikataba hiyo kwa niaba ya Wizara wakati Mwanzilishi wa IYF Mchungaji Ock Soo Park ambaye pia ni Mchungaji Mwandamizi wa kanisa la Good News Gangnam la nchini Korea ametia saini kwa niaba ya IYF.
Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara.
Pamoja na utiaji saini wa mikataba hiyo ya Ushirikiano, Mchungaji Ock Soo Park pia alitoa tuzo ya kuthamini mchango wa kazi azifanyazo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.
Akizungumza baada ya utiwaji huo wa saini, Dkt. Fenella alitoa shukrani zake za dhati kwa Kikundi cha IYF kwa kazi nzuri wanazozifanya za kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wa kitanzania ambayo yanawawezesha vijana wengi kubadilika fikra zao kutoka hasi kuwa chanya.Pia alimshukuru Mchungaji Ock Soo kwa tuzo aliyompatia.
Kikundi cha vijana cha IYF kimekuwa kikiendesha kambi zake nyingi hapa nchini ambazo zinaandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kauli mbiu ya kambi hizo kwa mwaka huu ni “Badilisha Fikra kutoka mtazomo hasi kuwa chanya”
No comments:
Post a Comment