Monday, August 05, 2013

Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton Atua Dar Kiaina

 
Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton pia alitembelea moja ya saluni ya kutengenezea nywele ya Bi Zainabu Rashidi (kulia) ambaye ni mmoja wa wanakikundi cha Upendo Hisa Group cha Vingunguti Mtambani, DSM jana.
 Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akizungumza na wanachama wa Upendo Hisa Group alipotembelea kikundi hicho kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Meneja Miradi wa Shirika la kimataifa la Plan International Bw Paul Lusato na Catherine French Mkuu wa wafanyakazi ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Barclays.
  Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton  akipanda gari muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete IKULU Jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Shabani Tolle na Mwananchi
----
 Rais wa Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton jana alifanya ziara katika makazi ya watu duni eneo la Vingunguti, wilayani Ilala Dar es Salaam, ambapo alikagua miradi midogomidogo ya wananchi inayofadhiliwa na mfuko wake (Bill Clinton Foundation).

Clinton alitembelea eneo hilo akitokea moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za Afrika kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.
Katika eneo hilo rais huyo mstaafu alipokewa kwa shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku baadhi ya wananchi wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi huyo kutembelea makazi yao.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...