Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.
Hata
hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa
alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na
Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na
fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
Kamati
pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na
anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo.
Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
Vilevile
Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji,
kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala
hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).
Kwa
upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi
watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya
kazi nchini (work permits).
Kamati hiyo itakutana tena
Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe
zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo
hazikuafikiana.
SOURCE:SHAFII
DAUDA
No comments:
Post a Comment