Wednesday, August 07, 2013

UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA WAWAKA MOTO ASUBUHI HII


Moto mkubwa unaripotiwa kuzuka asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) jijini Nairobi.

Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika na juhudi za kuuzima zinaendelea, ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vipo uwanjani hapo kuthibiti janga hilo.

Uwanja huo hivi sasa umefungwa na hakuna ndege kutua ama kuruka isipokuwa kwa dharura tu.

Moto huo unasemekana ulianza majira ya saa 11 za alfajiri sehemu za idara ya uhamiaji na kusambaa katika eneo la abiria wa kimataifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anaripotiwa kuelekea uwanjani hapo hivi sasa kukagua janga hilo, na habari zinasema hakuna mtu aliyedhurika kwa moto huo ingawa hasara iliyopatikana inasemekana ni kubwa na kwamba abiria wengi wamekwama uwanjani hapo. Barabara kuu ya kuelekea JKIA imefungwa.

Tutaendelea kuwaletea habari zaidi kadri zitavyozidi kupatikana

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...